Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PADRE PAUL HAULE AFARIKI DUNIA



Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Petro ‘St Peters’ jijini Dar es Salaam, Paul Haule, amefariki dunia Agosti 18, 2021 saa 10:30 jioni wakati akitibiwa katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa iliyopo Ukonga jijini Dar es salaam.

Taarifa za awali zinasema mwili wa Padre Haule ambaye alikua amelazwa kwa siku kadhaa umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Mbali na kuwa paroko msaidizi, Padre Haule alikuwa mkurugenzi wa matangazo Radio Tumaini.

Tumuombee apumzike kwa amani.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com