Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imeahirisha usikillizaji wa ushahidi wa shahidi namba saba upande wa Jamhuri wa kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kutokana na Mshtakiwa namba Moja Ole Sabaya kutokufika mahakamani kutokana na sababu za kiafya.
Akiahirisha shauri Hilo Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo amesema shauri hilo litaendelea kesho Agosti 05 asubuhi kwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa shahidi namba saba Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Gwakisa Minga ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Arusha.
Social Plugin