Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi waJamii, Ofisi ya Rais -Tamisemi Rasheed Hamisi Maftah akizungumza wakati wa kikao cha siku moja cha kutoa matokeo ya tathmini ya afua za dawa za kinga- tiba dhidi ya Malaria kwa watoto wa shule msingi kwenye maeneo yenye maambukizi makubwa iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa Binadamu (NIMR) kituo cha Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Tanga Dk Mercy Chiduo akizungumza wakati wa kikao hicho |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dkt Paul Kazyoba akizungumza wakati wa kikao hicho |
Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Sebastian Masanja akizungumza wakati wa kikao hicho |
Mwakilisho wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) akizungumza wakati wa kikao hicho |
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi waJamii, Ofisi ya Rais -Tamisemi Rasheed Hamisi Maftah amesema Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ofisi ya Rais-Tamisemi taasisi mbalimbali za Utafiti na wadau mbalimbali hadi kufikia mwaka 2030 itakuwa imetokomeza ugonjwa wa malaria nchini kwa kutumia afua mbalimbali.
Maftaha aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati wa katika kikao cha siku moja cha kutoa matokeo ya tathmini ya afua za dawa za kinga- tiba dhidi ya Malaria kwa watoto wa shule msingi kwenye maeneo yenye maambukizi makubwa iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa Binadamu (NIMR) kituo cha Tanga.
Maftah ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi amesema kuwa kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia mpango wa kudhibiti Malaria (NMCP), Ofisi ya Rais-Tamisemi na wadau mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huu kiwango cha maambukizi kimeendelea kushuka kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14.5 mwaka 2015 hadi asilimia 7.5 mwaka 2017 pia idadi ya vifo imepungua kwa kiwango kikubwa.
Alisema pamoja na mafanikio hayo makubwa,malengo ya kitaifa ni kuhakikisha kiwango cha malaria kinafikia chini ya asilimia 3 ifikapo 2025 na kutokomeza kabisa ugonjwa huu ifikapo 2030.
Mkurugenzi huyo alisema ili kufikia malengo hayo wanahitaji kuongeza ufanisi zaidi kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisayansi zinazotokana na tafiti mbalimbali,kuboresha mbinu za utekelezaji wa afua kinga mbalimbali za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Tanga Dk Mercy Chiduo amesema kituo hicho kwa kushirikiana na mdau Chuo Kikuu cha Antiwerp cha Ubelgiji mwaka 2019-2021 walifanya utafiti uliolenga kutathmini ufanisi wa afua ya dawa za kinga- tiba dhidi ya malaria kwa kundi la watoto wenye umri wa kwenda shule wa miaka 5-15 ambao wamekuwa na maambukizi makubwa lakini hawaoneshi dalili ambao wamekuwa ni chanzo cha maambukizi kwa jamii nzima na mwaka 2020 hadi 2021 NIMR kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) walifanya utafiti huo katika halmashauri za Handeni Mji, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Kilindi ambao dawa hizo zimeonesha matokeo mazuri.
Naye Mtafiti Mkuu NIMR -Tanga,Dk Geofrey Makenga amesema kuwa NIMR kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Tamisemi,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) walifanya utafiti huo katika halmashauri za Handeni Mji, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Kilindi kwa kujumuisha shule 127 zenye wanafunzi 90,000 ambapo wakuta maambukizi ya malaria kwa watoto wa shule ni asilimia 48 Handeni Vijijini, asilimia 18 Handeni Mji na asilimia 20 Kilindi ambapo baada ya kupewa dawa hizo zilionesha matokeo chanya.
Social Plugin