Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akifungua Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Muwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Ephraim Simbeye,akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula,akitoa utambulisho wa viongoiz wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako (hayupo pichani ) mara baada ya kufungua Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Kaimu rais wa chama cha maafisa maendeleo ya jamii hapa nchini Bw.Wanchoke Chinchibera,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiagana na washiriki mara baada ya kufungua Mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Halmashauri za Tanzania bara Kuhusu Masuala ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma.
.......................................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imepanga kutumia Shilingi bilioni 43 kwa ajili ya kuanzisha vituo atamizi lengo likiwa ni kuendeleza teknolojia na ubunifu katika Taasisi na Vyuo Vikuu nchini.
Hayo ameyasema leo Agosti 30,2021 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote hapa nchini kikao chenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuibua na kuzitambua bunifu za teknolojia katika maeneo yao ya kazi.
“Sisi kama serikali tuna tambua mchango mkubwa wa bunifu za teknolojia kwa mwaka huu wa fedha sisi tumetenga bilioni 43 hizi zitakwenda kuboresha mazingira na kutumika kuwaendeleza wabunifu katika vituo atamizi vilivyopo katika vyuo vikuu mbalimbali,
Waziri Ndalichako amesema kuwa tuna vyuo kama Chuo Kikuu cha Dar es saalam UDSM, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Mandela, Mzumbe, na Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya MUST ni miongoni vya vyuo ambavyo vinatumika kulea wabunifu tunaowaibua katika mashindano ya MAKISATU.
Aidha Waziri Ndalichako ametoa wito kwa wabunifu kuendelea kujitokeza ili ubunifu wao utambuliwe na kuendelezwa kupitia vituo hivyo.
“Lakini pia nichukue nafasi hii kuziagiza Taasisi zinazohusika na masuala ya teknolojia na ubunifu nchini kuongeza kasi ya kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu wachanga na kuwajengea uwezo stahiki na kuhakikisha kwamba bunifu zao zinalindwa ipasavyo,”amesema Prof. Ndalichako.
Prof.Ndalichako amesema kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ni kiungo muhimu katika kuwaibua, wabunifu wachanga hasa wale wa mfumo usio rasmi ndio maana Wizara yake ndio maana imewapa mafunzo yatakayowawezesha kushiriki katika masuala ya ubunifu kwa kujiamini zaidi.
“ Ndio maana tumewaita hapa ninyi ndio mnakuwa na watu tangu ngazi za chini tunaamini kupitia kwenu tunaweza kupata wabunifu wengi sana hasa wabunifu ambao wapo nje ya mfumo rasmi ninyi mnaweza kuwapata kiurahisi” amesema Prof.Ndalichako
Amesema mafunzo haya yanafungua ukurasa mwingine katika juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana na wadau wote muhimu katika kulipa msukumo zaidi eneo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
“Wizara yangu imedhamiria kupanua wigo wa wadau wa kuhamasisha matumizi na maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa kwa wananchi wanaoishi vijijini,”amesema.
Prof.Ndalichako amesema Serikali inatambua umuhimu na mchango wa teknolojia na ubunifu katika kurahisisha maisha kwa kuokoa muda unaotumika katika utendaji kazi, kuongeza tija na ubora katika uzalishaji wa bidhaa na hata katika utoaji huduma.
“Ubunifu ukitumika vyema, ni nyenzo na kichocheo cha maendeleo ya haraka katika sekta mbalimbali kama vile elimu, viwanda, afya, madini, nishati, usafirishaji, utalii, kilimo na mifugo ubunifu unawezesha kuzalisha bidhaa kwa wingi na kutoa huduma bora kwa wananchi,”amesema.
Amesema katika jitihada za kuhamasisha ugunduzi na ubunifu wa teknolojia zinazolenga kutatua changamoto katika jamii ya watanzania, mwaka 2019 Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ilianzisha Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, maarufu kwa jina la “MAKISATU”.
''Lengo kuu la kuanzisha Mashindano haya ni kuibua na kutambua ubunifu na teknolojia mahiri zilizozalishwa na vijana wa Kitanzania,kukuza hamasa ya ubunifu,kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii,kuchochea ugunduzi na ubunifu wa kisayansi na teknolojia utakaotegemeza maendeleo ya uchumi wa viwanda''amesema Prof.Ndalichako
Waziri Ndalichako amesema Katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza kwa Mashindano hayo jumla ya wabunifu na wagunduzi wa teknolojia mbalimbali zinazozalishwa nchini wapatao 1,785 waliibuliwa na kutambuliwa na Wizara.
Aidha, wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ili ubunifu wao uweze kufikia hatua ya kubiasharishwa na hivyo kuongeza kipato na fursa za ajira kwa vijana.
Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, imetambua na kuhakiki teknolojia zilizozalishwa na vijana wa kitanzania zipatazo 389 na taarifa zake kuingizwa kwenye kanzidata ya Wizara inayohusu utafiti na ubunifu.
Aidha amesema baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa ukusanyaji na uhakiki wa taarifa za teknolojia na bunifu zilizotambuliwa ni pamoja na Ukusanyaji hafifu wa taarifa za wabunifu kutoka ngazi za Wilaya, Kata, Vijiji na Mitaa na mwitikio hafifu wa baadhi ya wabunifu katika zoezi la utambuzi teknolojia na ubunifu na hata kushiriki MAKISATU.
“Changamoto hizo zilichangiwa na uelewa mdogo kuhusu dhana nzima ya teknolojia na ubunifu na umuhimu wa kutoa taarifa sahihi za wabunifu hao.Kwa kuwa, kazi ya kutambua teknolojia na uendeshaji wa MAKISATU ni endelevu, Wizara imeona ni vema kuandaa mafunzo haya kwenu Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Halmashauri ili kuwa uelewa wa pamoja,”amesema
Aidha amesema Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha ubunifu unapewa kipaumbele cha hali ya juu katika kuharakisha maendeleo kijamii na kiuchumi.
“Wizara yangu itaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuendeleza ubunifu nchini, kupitia vituo vya kuendeleza teknolojia na ubunifu vilivyopo na kuendelea kuanzisha vingine vipya. Mathalani, kupitia mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET),”amesema.
Awali Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amesema kuwa anaamini kwa msaada wa maafisa maendeleo ya jamii kupitia mafunzo hayo wataweza kuwa na wigo mpana zaidi wa kuibua teknolojia mbalimbali hapa nchini.
''Tutaendelea kutoa mafunzo kama hayo hadi kwa maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata, na tulianza na maafisa maendeleo ngazi za Mikoa na sasa halmashauri tunaamini kuwa tutafika hadi ngazi za kata''amesema Prof.Mdoe
Kwa upande wake Kaimu rais wa chama cha maafisa maendeleo ya jamii hapa nchini Bw. Wanchoke Chinchibera amesema baada ya kupata mafunzo hayo watakwenda kulifanya jukumu hilo kwa ufasaha mkubwa kuhakikisha wanawaibua wabunifu wengi wa teknolojia kwa maendeleo ya taifa.
“Tuwahakikishie kuwa tutakwenda kuifanya kazi hii kiufasaha na tutakwenda kuhamasishana kupitia chama chetu kuhakikisha tunaibua bunifu nyingi katika maeneo yetu ya kazi” amesema Wanchoke.