Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YASITISHA UAGIZWAJI WA MBOLEA KUPITIA MFUMO WA UNUNUAJI WA PAMOJA

 

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Nkenda 

Na Magreth Katengu - Dar es salaam

Wizara ya Kilimo imesitisha uagizwaji wa mbolea kupitia mfumo wa ununuzi wa pamoja (bulk procurement) huku akisema Makampuni hayo yanaruhusiwa kuingiza Mbolea hizo kwa wingi nchini bila kutumia mfumo huo.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Nkenda wakati akizungumza katika kikao kazi cha wadau wa mbolea nchini ambapo amesema mbolea inayoingia kwa mfumo wa Bulk ni kidogo ukilinganisha na mbolea inayoingizwa nchini nje ya mfumo hali inayosababisha kutokidhi mahitaji ya wakulima.

"Biashara ya mbolea ni kwa sasa ni huria mfanyabiashara anaweza kununua mbolea popote duniani na kuuza popote duniani", amesema Profesa Nkenda.

Profesa Nkenda amesema Uongozi wa Bandari imeahidi kutoa kipaumbele cha kushusha mbolea inayoingia nchini pamoja na kutatua changamoto ya ukosefu wa vifaa za kupakua mbolea hiyo.

Hata hivyo, Profesa Nkenda amesema Wizara ya Kilimo inatarajia kufufua Kampuni ya mbolea Tanzania ili kusaidia uzalishaji wa mbolea nchini huku akisema Wizara itamuomba Rais Samia kumteua mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo ili kuendeleza uzalishaji wa mbolea.

Profesa Nkenda amewashukuru Makampuni ya uzalishaji wa mbolea Nchini kwa kukubali kpunguza gharama ya mbolea kwa wakulima.

Aidha kupitia majadiliano hayo ya leo yatatoa suluhisho la kushusha gharama ya ununuaji mbolea kwa wakulima .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com