Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Baraza la vyama vya siasa nchini limesema litahakikisha Viongozi wote wa vyama vya siasa wanafanya siasa za kizalendo,amani, utulivu na kujenga democrasia kwa kizazi cha sasa na kijacho kisichokuwa na chuki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi kamati za uongozi mbalimbali za baraza hilo, Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa, Juma Khatibu amesema wanahitaji kujenga usawa wenye ,misingi ya demokrasia makini na kuweka mbele zaidi uzalendo na si siasa za chuki ambazo hubomoa taifa.
"Kamati hizi tulizoziweka zitahakikisha mpango mkakati ni kijenga Taifa la kizalendo lenye amani na utulivu huku siasa za kistaarabu zikifanyika kwa ustaarabu",aliaema Khatibu.
Aidha amesema wameunda kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha,maadili ,sheria ikiwa na matarajio ya kufanyakazi kwa pamoja na vya vyote bila ubaguzi katika kujenga Tanzania imara kiuchumi na kiplomasia.
Social Plugin