Kulia ni Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Frank Nguyu ambaye ni Afisa Mikopo wa SIDO Mkoa wa Shinyanga akiangalia shughuli ya uoakaji mikate wakati akifunga mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development wameendesha mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa kipindi cha siku 7 katika kata ya Old Shinyanga na kufungwa leo Jumamosi Agosti 14,2021 Mjini Shinyanga kwa kufanya shughuli za Uokaji Mikate, Skonzi na Keki katika kiwanda cha Mikate cha Albany Bakery kinachomilikiwa na Robert Martine kinacholelewa SIDO Mkoa wa Shinyanga.
Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Frank Nguyu ambaye ni Afisa Mikopo wa SIDO Mkoa wa Shinyanga amewataka vijana hayo kutumia ujuzi waliopewa katika mafunzo hayo na kwamba SIDO itaendelea kuwa karibu nao ili kuhakikisha wanainuka kiuchumi.
“Nendeni mkatumie mafunzo haya mliyopewa, katumieni vifaa vilivyotumika katika kuwafundisha masuala ya Uokaji Mikate, Skonzi na Keki. Sisi SIDO kipaumbele chetu ni kazi za mikono, tunapenda kuona wajasiriamali wanajikwamua kiuchumi na kuwasaidia wananchi kupata Kipato. Mnachotakiwa kufanya sasa ni kujua namna ya kutengeneza faida kupitia kazi mnazofanya”,amesema Nguyu.
Awali akizungumza, Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban amesema mafunzo hayo yametolewa kwa kikundi cha Vijana Mabinti 10 kutoka kata ya Old Shinyanga maarufu ‘Girls Power’ ambao wamefundishwa namna ya Uokaji pamoja na kupewa mafunzo kuhusu huduma zinazotolewa na SIDO, Usimamizi wa Biashara,huduma za fedha,masoko na uendelezaji wa Teknolojia.
“Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na kuitumia SIDO kama nyenzo na daraja la mafanikio kwenye ujasiriamali”,amesema Taban.
Kwa upande wake Kijana wa Kujitolea kutoka Shirika la Restless Development, John Eddy amesema vijana hao mabinti wameanzisha kikundi chao kiitwacho Girls Power ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa ‘Vijana Tunaweza’ unaotekelezwa na shirika la Restless Development kwa ufadhili wa UNFPA wenye lengo la kuwawezesha vijana mabinti kiuongozi na kiuchumi.
“Mradi huu unatekelezwa katika kata tatu ambazo ni Ndembezi, Ndala na Old Shinyanga . Jumla ya mabinti 30 wanashiriki katika mradi huu ambapo kila kata tumechukua mabinti 10. Walioshiriki katika mafunzo haya ni wale wanaotoka katika kata ya Old Shinyanga waliokubaliana kuanzisha kiwanda cha Bakery”,amesema Eddy.
Aidha ameipongeza SIDO kwa kutoa mafunzo kwa vijana hao ambayo yawasaidia kujiinua kiuchumi.
Kwa upande wao mabinti hao akiwemo Janeth Titus wameshukuru kwa mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi na kutumia vifaa vya mwanzo walivyopewa na SIDO kuanzisha mradi wao wa Kiwanda cha Bakery.
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Frank Nguyu ambaye ni Afisa Mikopo wa SIDO Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Frank Nguyu ambaye ni Afisa Mikopo wa SIDO Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Kijana wa Kujitolea kutoka Shirika la Restless Development, John Eddy akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Kulia ni Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Frank Nguyu ambaye ni Afisa Mikopo wa SIDO Mkoa wa Shinyanga akiangalia shughuli ya uoakaji mikate wakati akifunga mafunzo ya Usindikaji Vyakula (Uokaji – Bakery) kwa vijana kutoka Kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga wanaotarajia kuanzisha Kiwanda cha Uokaji (Bakery).
Mmiliki wa kiwanda cha Mikate cha Albany Bakery Robert Martine kilichopo Kambarage Mjini Shinyanga akiwafundisha vijana mabinti kutoka kikundi cha Girls Power namna ya kutengeneza Skonzi
vijana mabinti kutoka kikundi cha Girls Power wakitengeneza Skonzi
Mmiliki wa kiwanda cha Mikate cha Albany Bakery Robert Martine kilichopo Kambarage Mjini Shinyanga akiwafundisha vijana mabinti kutoka kikundi cha Girls Power namna ya kutengeneza Skonzi
Kikundi cha Girls Power wakiendelea na shughuli ya kutengeneza Skonzi
Shughuli ya kutengeneza Skonzi ikiendelea
Vijana wakitengeneza Keki
Janeth Titus akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga mafunzo hayo
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin