Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, imeahirishwa hadi kesho Agosti 6, 2021, kutokana na muonekano hafifu wa video conference, kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo huo, ambapo kesho atafikishwa mahakamani majira ya saa 3:00 asubuhi.
Kesi hiyo ya ugaidi ilikuwa itajwe leo Agosti 5, 2021, ambapo Mbowe na wenzake walikuwa katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam lakini kutokana na matatizo ya mtandao ilishindwa kuendeshwa vizuri.
Akizungumza hii leo mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala, amesema kuwa, "Teknolojia imefeli hivyo tumeshindwa kufanikisha mchakato huo kwa sababu kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya video conference facility za hapa katika Mahakama ya Kisutu na Gereza la Ukonga na tumekubaliana kwamba kesho washtakiwa waletwe mahakamani".
Social Plugin