Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Bw.Luciana Segesela,akiwasilisha taarifa kuhusu ukarabati wa chuo hicho, Ununuzi/ugawaji wa vifaa mbalimbali pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum kwa ajili ya uboreshaji wa Elimu nchini kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Wanafunzi wa Chuoa cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakimsikiliza Mkuu wa Chuo hicho Luciana Segesela,akiwasilisha taarifa kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho kuhusu ukarabati wa chuo hicho, Ununuzi/ugawaji wa vifaa mbalimbali pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum kwa ajili ya uboreshaji wa Elimu nchini
Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Chuoa cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Luciana Segesela,wakati akiwasilisha taarifa kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho kuhusu ukarabati wa chuo hicho, Ununuzi/ugawaji wa vifaa mbalimbali pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum kwa ajili ya uboreshaji wa Elimu nchini
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakiimba wimbo maalum.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Bw.Luciana Segesela,akionyesha miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika chuo hicho kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mratibu Taaluma Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Lucas Nkivuyo,akitoa maelezo kuhusu mashine zinazotumika kwa wanafunzi wasio na usikivu kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mwanachuo wa Mwaka wa Pili idara ya wasioona Amour Athumani mwenye ulemavu wa kutosikia akionyesha kifaa wanachotumia katika kuwasiliana na kujisome vilivyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Bw.Luciana Segesela,akiwa na Waandishi wa Habari wakiendelea na kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakiwa katika chumba cha Computer wakijisomea mara baada ya kupokea vifaa bora kabisa kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakiwa katika chumba cha Maktaba wakijisomea mara baada ya ukarabati pamoja na kuletewa vifaa mbalimbali katika chuo hicho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Ujenzi wa jengo la Maabara ya Sayari ukiendelea.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Maktaba.
Muonekano wa shule ya Sekondari Elimu Maalum Patandi,iliyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
.........................................................................................
Na Alex Sonna,Arusha
CHUO cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Mkoani Arusha kimeelezea mafaniko 15 ambayo imeyapata mara baada ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kufanya ukarabati mkubwa katika chuo hicho ikiwemo kuleta mabadiliko chanya kwa kuongeza fursa na kuinua ubora wa elimu.
Akiongea na Waandishi wa Habari waliotembelea chuoni hapo kuona miradi inayotekelezwa na Taasisi hiyo,Mkuu wa Chuo cha Ualimu Maalum Patandi,Luciana Segesela amesema maboresho yaliofanywa na serikali katika sekta ya elimu kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia hususani kwenye vyuo vya Ualimu yameleta mabadiliko chanya kwa kuongeza fursa na kuinua ubora wa elimu.
Vilevile amesema imesadia kuongeza morali ya kazi kwa wafanyakazi kutokana na kufanyia kazi katika mazingira rafiki na salama.
Pia,amesema imesaidia uwepo wa utoaji wa elimu bora na kuongeza ufaulu katika mitihani kwani chuo hicho kimepata ufaulu wa juu na hakunamwanachuo aliyefeli katika mtihani wa taifa.
“Imeongeza uwezo wa chuo wa kudahili wanachuo kutoka idadi ya wanachuo 260 hadi 450.Imeendelea kuongeza ari ya ujifunzaji kwa wanafunzi kupitia uwepo wa vifaa mbalimbali vya kujifunzia ikiwepo vitabu. Tuna Imani hata majengo ya makataba na maabara yanayojengwa yakiisha yataweza kuchochea zaidi ari hii ya ujifunzaji kwa wanachuo na wanafunzi,”amesema Segesela
Aidha ameongeza kuwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wenye mahitaji maalumu umeleta ukombozi na matumaini makubwa kwa Chuo hicho kwani walimu tarajali wamepata sehemu ya kufanyia mafunzo kwa vitendo
"shule hii inaendelea kutoa fursa chuoni kwa wakufunzi na wanachuo kufanya tafiti mbalimbali na kutekeleza mafunzo kwa vitendo kulingana na masomo na idara zao kila inapohitajika" amesema Segesela
Amesema kuwa ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia umesaidia chuo kuweza kuandaa wanachuo wanaoendana na stadi za karne ya ishirini na moja na mapinduzi ya viwanda ya awamu ya nne kwa kupitia uwepo vifaa mbalimbali vya ufundishaji na ujifunzaji vilivyoletwa ikiwa ni pamoja na kusaidia ufundishaji wa TEHAMA kwa kutumia komputa tulizopata na mafunzo waliyopata wakufunzi.
Vilevile,imeondoa changamoto kwa wanachuo na watumishi wenye mahitaji maalumu ya kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine kutokana na kuwepo kwa mazingira rafiki kwao kupitia ujenzi wa njia za kutembelea kwa paving blocks.
“Kuwepo kwa huduma ya uhakika ya maji safi kupitia uchimbaji wa kisima kirefu cha maji ambacho kimetatua changamoto kubwa ya tatizo la muda mrefu la maji chuoni na sekondari,”amesema
Pia,Uwepo wa usafiri wa ukakika umesaidia kurahisisha utekelezaji wa shughuli za chuo na huduma kwa wanachuo ikiwemo kuwapeleka wagonjwa hospitalini.
“Chuo kimeongeza fursa ya mahusiano na taasisi zingine pamoja na mamlaka za serikali ya wilaya na mkoa kwa chuo kuwezesha kufanikisha shughuli zao mbalimbali kwa kutumia miundombinu na vifaa vya chuo.
Aidha,Patandi imekuwa kitovu cha kujifunza kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuhusu masuala mbalimbali ya watu wenye mahitaji maalumu na namna ya utoaji wa huduma rafiki kwao.
“Kuboresha madhari na mazingira ya chuo kwani chuo kinaonekana kipya.Ujenzi wa uzio wa chuo umesaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na wanajumuiya ya chuo Pamoja na kudhibiti suala la nidhamu ya wanachuo kwa kudhibiti utoro,”amesema.
ZAIDI YA BILIONI 1.1 ZAKARABATI MIUNDOMBINU PATANDI
Katika hatua nyingine,Mkuu huyo wa Chuo amesema zaidi ya shilingi bilioni moja zimetumika kukarabati madarasa,mabweni,bwalo,jengo la utawala,mifumo ya umeme,pamoja na kuboresha maabara ya upimaji wa watoto wenye mahitaji maalum,katika Chuo cha Ualimu elimu maalum Patandi Mkoani Arusha.
Amesema serikali kupitia wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekuwa ikikifanyia ukarabati chuo kwa awamu tofauti tofauti pamoja na kuongeza miundombinu mingine ya chuo ili kukidhi mahitaji.
Mkuu huyo wa Chuo amesema ukarabati huo ni wa madarasa,mabweni,Ujenzi wa njia za kutembelea kwa paving blocks,Ukarabati wa bwalo na jiko la chuo,Ujenzi wa choo kipya cha wanaume chenye matundu 15 Na mabafu 15,Ukamilishaji wa ujenzi wa uzio wa chuo Pamoja na geti lake.
Vilevile,ukarabati wa jengo la utawala linalotumika sasa,ujenzi wa jingo jipya la utawala wa chuo,ukarabati wa mifumo yote ya umeme,mifumo ya zamani na ujenzi wa mifumo mipya ya maji safi na maji taka,kuboresha maabara ya upimaji wa Watoto wenye mahitaji maalumu.
“Thamani ya ukarabati huu, kwa ujumla wake pamoja na shughuli zinazoendelea kumaliziwa sasa ni jumla ya gharama ya shilingi bilioni 1,171,157,613.29,”amesema Mkuu huyo wa Chuo.
MWAKA 2013-2014 ILITOA BILIONI 1.6
Amesema kwa mfano mwaka 2013/2014 Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia iliboresha miundombinu ya chuo kwa kujenga mabweni mawili mapya, kuchimba kisima cha maji pamoja na kujenga sehemu ya uzio wa chuo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.6,Mradi ambao ulitekelezwa na Mkandarasi Suma JKT.
“Kuanzia mwaka 2017 mwishoni wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imefanya jitihada kubwa kukarabati na kuboreshaa miundombinu ya chuo ambayo kwa ujumla wake ukarabati huo umekifanya chuo cha Patandi kuonekana kipya kabisa na hivyo kuwa na mazingira mazuri ya ufundishaji na ujifunzaji.
“Kwa sasa chuo kinaendelea na utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa chuo kwa kushughulikia miundombinu ifuatayo,Kumalizia ujenzi wa jengo la utawala wa chuo, Kumalizia ujenzi wa njia za kutembelea kwa miguu kuelekea mabwenini kwa paving blocks,”amesema.
Vilevile,kujenga maktaba yenye huduma za TEHEMA ndani yake yenye uwezo wa kupokea wanachuo zaidi ya 250,Kujenga maabara ya sayansi ya masomo ya kemia na bailojia
“Kwa ujumla Shughuli zote hizi za ukarabati wa chuo zimetekelezwa kwamfumo wa Force Account chini ya usimamizi wa washauri elekezi kutoka huo Kikuu cha Sayansi cha Mbeya (MUST),”amesema.
Amesema Chuo hicho kina wanafunzi wa mwaka wa pili 175 (me-84 na Ke-91) na wanachuo wa mwaka wa kwanza waliopangwa ni 259 (me- 122 na ke- 137) ambapo kwa ujumla wapo wanachuo 434 (ME ni 206 na KE 228).
WAPOKEA VIFAA KUTOKA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Bw.Segesela amesema wamefanikiwa kupokea vifaa mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,ambavyo vilinunuliwa kwa nyakati tofauti.
Amevitaja vifaa hivyo ni pamoja na gari jipya aina ya landcruiser hard top,Kuletewa vitabu vya aina mbalimbali zaidi ya nakala 770,kuletewa computer 30 aina ya desk zilizokamilika na zingine 20 zipo katika hatua ya kumilishwa mchakato wake,kuletewa mashine ya photocopy machine (heavy duty) moja,pamoja na projecta tano.
Pia,kununuliwa vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia wanafunzi wenye ulemavu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 138,kuletewa vitabu mbalimbali vya baadhi ya masomo ya kidato cha kwanza na cha pili kwa ajili ya shule ya sekondari,Kuletewa viti mwendo vitatu kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari wenye mahitaji maalum.
“Pamoja na mapokezi ya vifaa hivyo, pia wafanyakazi wa chuo wamepatiwa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea ujuzi katika maeneo yao ya taaluma na masuala ya mtambuka kulingana na kada/taaluma zao kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao,”amesema.
SHULE YA SEKONDARI PATANDI
Kuhusiana na Mpango wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi,Mkuu huyo amesema ulilenga kujenga majengo kumi ambayo ni utawala,bwalo,jiko,madarasa manne na mabweni manne.
“Bloko za Madarasa zilizojengwa zina jumla ya vyumba 12 na ofisi 6 pamoja na vyumba ambavyo vinaweza kutumika kwa ajili ya komputa, maktaba, maabara ya sayansi 1. Pia bloko za mabweni zina vyumba 14 kila moja ambavyo vinaweza kuchukua wanafunzi 4 hadi 6 kila chumba na ukumbi wa bwalo unakadiriwa kuchukua wanafunzi 300 hadi 400 ikitegemea mpangilio wa ukaaji katika vyumba utakavyowekwa,”amesema.
Amesema hadi kufikia Agosti mwaka 2021 ujenzi wa majengo hayo yote kumi umekamilika kwa wastani wa asilimia zaidi ya 99.9%.
WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA YANUNUA THAMANI
Mkuu huyo wa Chuo amesema Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia imefanikiwa kununua na kutengeneza samani za shule ambazo ni Vitanda double ‘decker‘ 68 sawa na single 136,viti vya wanafunzi darasani 185,meza vya wanafunzi darasani 185,meza za bwalo la chakula 65,viti vya bwalo la chakula 400
Pia,utengenezaji wa viti vya ofisini 18,viti maalum vya ofisi 3,Meza kubwa ya ofisini,Kabati 1 ya usajili ‘Steel waiting chairs (three seaters)’,Meza ya mbao ya ofisini (std) 3,Kiti (std) cha mbao 1,Magodoro 136.
Social Plugin