Katibu Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,Kenani Kihongosi akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2021 Jijini Dodoma wakati akitangaza kuanzisha Ligi ya Vijana itakayoitwa UVCCM Green Cup 2021.
…………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) inatarajia kuanzisha Ligi ya vijana itakayoitwa UVCCM Green Cup ambayo itajumuisha vijana wa nchi nzima lengo likiwa ni kuibua pamoja na kuviendeleza vipaji hivyo.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 24,2021 Jijini Dodoma na Katibu wa UVCCM Taifa,Kenani Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema ligi hiyo itaitwa UVCCM Premium Cup ambayo itachezwa Tanzania Bara na Visiwani.
“Kama umoja wa Vijana tumeanzisha Ligi ya Mpira ya vijana itaitwa UVCCM Premium Cup na itachazwa Tanzania Bara na Visiwani,tunaenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ukisoma kifungu cha tatu sura ya 81 kinaelezea masuala ya michezo”amesema Kihongosi
Hata hivyo Kihomgosi amesema kuwa michezo ni ajira na fursa na katika michezo kuna wasanii wakubwa kina Diamond na Ally Kiba wanaitangaza nchi yetu kwa kupitia Sanaa tunawachezaji kina Samatta,Msuma na wengine wameweza kupata kipato kupitia michezo
Bw.Kihongosi amesema anaamini kupitia ligi hiyo wataweza kuibua vipaji na kufungua fursa za vijana mbalimbali wenye vipaji ambao hawakuweza kuonekana.
“Tunaamini Ligi hii itaenda kufungua fursa za vipaji vya Tanzania na sisi Umoja wa Vijana wa CCM tunataka kuwaambia watanzania tunagusa kila ‘angle’ tutawashirikisha vijana wa ngoma, maigizo na Netbalii na vipaji vyote tutaviendeleza.,”amesisitiza
Social Plugin