VYAMA 11 VYA UPINZANI TANZANIA VYAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA SUALA LA CHANJO NA KATIBA MPYA


Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Doyo Hassan akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona
Katibu Mkuu wa Chama Cha DP, Abdul Mluya akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Corona
Viongozi wa Vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi Bungeni wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Corona

****
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

VIONGOZI wa Umoja wa Vyama vya Siasa ambavyo havina wawakilishi Bungeni wamesema wataendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu kuhusu kuwataka wananchi kuwa na subira katika mchakato wa Katiba mppya.

Umoja huo umesema wao msimamo wao katika mchakato wa Katiba mpya mbali ya kumuunga mkono wanappendekeza mchakato uanzie ulipoishia awali kwa wananchi kupiga kura ya maoni kwani mapendekezo ya Katiba mpya yalishafanyika ,hivyo hawaoni sababu ya kuanza upya kwani ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha DP Abdul Mluya amesema msimamo wao wanaunga mkono kauli ya Rais lakini hawaoni sababu mchakato wa Katiba Mpya kuanza upya na badala yake uanzie ulipoishia.

"Kuna uwezekano wa kuendeleza pale walipoishia katika mchakato wa katiba mpya kuliko kuanza upya uandishi wa katiba kwa maana utaweza kupoteza gharama kubwa fedha ambazo zingeweza kuendeleza miradi mingine nchini.

“Kwenye mchakato wa katiba tuliishia kwenye kura ya maoni (katiba pendekezwa) kwahiyo msimamo wetu tunasema kwamba kutokana na Dunia kuingia kwenye wimbi la ugonjwa wa korona uliopelekea kuyumba kwa uchumi hatuoni tija na afya kwa watanzania kama tutakwenda kuwaingiza kwenye suala uandishi wa katiba mpya kama ile iliyotumia zaidi ya bilioni 200.

"Kuna haja ya msingi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutuleta kura ya maoni tupige kura ili kupata katiba ambayo imeshatumia fedha za wananchi kuliko kuanza uppya mchakato wa kuandika katiba mpya.Haya sisi ndio maoni yetu na yaheshimiwe kama nasi tunavyoheshimu mawazo ya wengine,"amesema.

Aidha amesema wanamuunga mkono Rais Samia katika chanjo ya COVID-19 ambayo ni hiyari sio lazima,lakini vyama hivyo vinawahamasisha wananchi kupata chanjo hiyo kwa lengo la kukabiliana na janga la ugonjwa huo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Bw.Doyo Hassan amewataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuikosoa chanjo ya kujikinga na Uviko -19 kwani chanjo hiyo inatolewa kwa hiari na haina madhara yoyote.

Doyo amesema Rais kwa busara zake ameruhusu kutoa mwanya kwa Watanzania wanaotaka na wasiotaka lakini yeye alikuwa ni miongoni mwa waliotaka na wakachanja na sisi viongozi tumemuunga mkono Rais katika chanjo ya Uviko kwasababu suala la afya linamuhusu mtu mmoja mmoja lakini kama taifa ukipoteza nguvu kazi ya taifa lazima upoteze harakati za kukuza uchumi.

Kuhusu Katiba mpya, Doyo amesisiti vyama hivyo 11 wanataka mchakato wa Katiba uanze ulipoishia ili kuokoa fedha, maana wanaodai Katiba sasa wengine walikuwepo wakati wa mchakato wa awali wa Katiba inayopendekezwa ambayo ipo.

"Nchi imeingia gharama kubwa katika mchakato umekwenda na umefikia hapo.Kama wananchi wanataka Katiba basi twendeni tukaanzie hapo.Sisi vyama 12 tunaomba serikali sikivu ombi letu tuendelee na mchakato ambao awali ulikuwa umeishia,"amesema Doyo.

CHANZO - MICHUZI BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post