Jumla ya watu 207,391 wamepatiwa chanjo ya UVIKO - 19 nchini Tanzania kwa hiari iliyoanza kutolewa hivi karibuni katika vituo vya kutolea huduma zaidi ya 550 kwa Tanzania bara.
Katika taarifa kwa Umma leo 15 Agosti, juu ya maendeleo ya utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 kwa Wanananchi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kwa Katibu Mkuu (Afya), Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa:
Tathimini ya zoezi la utoaji chanjo tangu Mikoa yote izindue tarehe 04/08/2021, inaonesha mpaka kufikia tarehe 14.08.2021, jumla ya walengwa 207,391 wamepatiwa chanjo hiyo kwa hiari, kati ya hao waliopatiwa chanjo hiyo, walengwa 121,002 ni wanaume ambao ni sawa na asilimia 58 (58.3%) na Wanawake ni 86,389 sawa na asilimia 41 (41.7%).