WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, nchini Tanzania Dk. Dorothy Gwajima amewaacha na hamaki wakazi wa jiji la Mwanza mara baada ya kusema, baada ya yeye kuchanja chanjo ya UVIKO-19, mume wake ametesti ‘mitambo’ kwake na kukuta yupo ‘fiti’ kama mwanamke.
Ametoa kauli hivyo jana jijini Mwanza alipokagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou Toure ya Jijini Mwanza. Amesema chanjo haiathiri kitu chochote katika mwili ndio maana yeye yupo vizuri baada ya kuchanjwa chanjo hiyo na kuhimiza watu kwenda kuchanjwa, “Hakuna aliyechanjwa akageuka kuwa zombi.”
Kumekuwa na taarifa kinzani mbalimbali juu ya chanjo hiyo ya UVIKO 19, moja ni kutoka Serekalini inayohamasisha na kumtaka mwananchi kuchanjwa chanjo hiyo kwa kuwa ni salama na inaokoa maisha, lakini kauli nyingine ni iliyoibuliwa na Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye anahubiri kila kukicha kuwa chanjo hiyo Sio salama na Viongozi wengi wa Serikali nchini wanafanya maigizo kwenye kuchanjwa.
Kauli hiyo ya Askofu Gwajima ilimlazimisha Dk. Gwajima juzi kuliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) kumkamata na kumhoji mbunge huyo wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi wa nchi kuhusu chanjo ya Uviko 19.
Alisema Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo ambalo linaloivuruga wizara yake ya Afya na Serikali ya Jamhuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema wakati umefika kwa jamii kuachana na visingizio vinavyosababisha kuendelea kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto na badala yake kusimamia misingi ya upatikanaji wa haki.
Akizungumzia kuhusu kauli ya IGP Sirro kuhusu kumkamata Gwajima alisema; “IGP yuko sahihi, watu wasijikite hapa watengeneze ajenda ya kisiasa, ukitengeneza ajenda inayonihusu unajidanganya nitakuvua nguo mubashara, baada ya mimi kutamka hivyo yeye akasema ameyasikia kwenye mitandao lakini kawaida lazima tupeleke maandishi….” alisema Dk. Gwajima.