WAZIRI UMMY MWALIMU AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA ZOEZI LA UTENGAJI EKARI 500 KWA AJILI YA VIWANDA KILA HALMASHAURI



Na  Josephine Charles - Kahama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka wakuu wa mikoa kusimamia zoezi la utengaji wa ekari 500 za maeneo katika halmashauri zote nchini ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda na kutoa fursa za ajira kwa watanzania.

Agizo hilo limetolewa leo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga katika ziara ya kikazi inayojumuisha wakuu wa mikoa yote nchini Pamoja na makatibu tawala inayolenga kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda pamoja na upangaji wa miji katika vituo vyao vya kazi.

Amesema zoezi hilo linapaswa kutekelezwa haraka ili kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vikubwa na vidogo katika vituo vyao vya kazi ikiwa ni Pamoja na kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wazawa.


Awali akitoa ufafanuzi kuhusiana na maeneo ya uwekezaji, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Bw. Anderson Msumba amesema wamepata faida kubwa huku Zainab Telack Mkuu wa Mkoa wa Lindi akaeleza changamoto walizokabiliana nazo Kipindi hicho wakati alivyokuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.


Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa nchini mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amewataka wawekezaji wazawa kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha chakula cha Samaki.

Aidha ziara ya Wakuu wa Mikoa nchini,Makatibu Tawala wa Mikoa,baadhi ya Waganga Wakuu wa Mikoa pamoja na wadau wengine wa Maendeleo ambayo ilianza Jana katika Manispaa ya Kahama imehitimishwa leo katika Kijiji cha Chapulwa Kata ya Isagehe kwa kutembelea Viwanda vya Kutengeneza Vinywaji Baridi vikiwemo Soda,Maji na Juice,Kiwanda Cha Kuchakata Nafaka aina za Mpunga na Mahindi kwa ajili ya Kutengeneza Unga wa Lishe na Vyakula vya Mifugo ikiwemo Samaki,Pamoja na eneo la Zongomera ambalo limetengwa kwa ajili ya wajasiriamali wadogo nawa Kati ili kufanya Biashara zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post