Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa iliyofanyiwa ukarabati na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mkurugenzi wa Maktaba Tanzania Dkt.Mboni Ruzegela,akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa ukarabati wa Maktaba hiyo uliofanywa na Serikali Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maktaba ya Mkoa wa Iringa iliyofanyiwa ukarabati na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akikagua Maktaba ya Mkoa wa Iringa mara baada ya kuizindua baada ya kufanyiwa ukarabati pamoja na maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Muonekano wa Vitabu mbalimbali vilivyomo katika Maktaba ya Mkoa wa Iringa iliyozinduliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe baada ya kufanyiwa ukarabati pamoja na maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Muonekano wa Jengo la Maktaba ya Mkoa wa Iringa lililozinduliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe baada ya kufanyiwa ukarabati pamoja na maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
........................................................
Na Alex Sonna,Iringa
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imetumia zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 kufanya maboresho makubwa katika maktaba saba za mikoa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akizindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa ambayo imefanyiwa ukarabati, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe amesema ukarabati huo ulilenga kuinua ubora wa elimu nchini.
“Bodi ya Huduma ya Maktaba nchini ilikuwa na changamoto nyingi ambapo mwaka wa fedha wa 2020/2021 tumetenga zaidi ya bilioni 1.5, tukaamua kuanzia maktaba za Mikoa saba na Iringa ni mojawapo" amesema Profesa Mdoe.
Katibu Mkuu huyo amesema ukarabati wa maktaba ya Iringa umehjarimu milioni 150 kwa ajili ya kukarabati huo na kwamba kabla ya ukarabati hali haikuwa nzuri.
Prof Mdoe amesema lengo ni kuinua ubora wa elimu ambapo amesema serikali itaemdelea kukarabati maktaba zilizobaki ili kuhakikisha zote zinakuwa na mazingira mazuri.
Kuhusiana na Changamoto ya upungufu wa fedha, Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kadri hali itakavyokuwa nzuri zaidi watazidi kuboresha na kuleta fedha zaidi.
Kuhusu changamoto ya rasiliamli watu amesema : “Yote tunayachukua kubwa ni hili la mkongo wa Taifa haya ni masuala ambayo tunayachukua, tutaona jinsi ya kuyaboresha,
AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA UBUNIFU
Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka watumishi wa maktaba nchini kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao ili kurejesha utamaduni wa zamani wa watanzania kujisomea.
“Nawaomba muongeze ubunifu maktaba hizi zimejengwa siku nyingi wenzetu wa zamani waliona mbali lakini sisi wa kizazi hichi tumeanza kupoteza utamadini wa zamani,ningependa tuurudishe umuhimu wa kusoma fanyeni kazi kwa bidii tupo kwa pamoja,” amesema Prof Mdoe.
Amesema Wizara hiyo ina taasisi 35 ambapo Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vipo 54 na zililetwa mwaka 2015-2016 kutoka Wizara ya Afya.Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Pia, amesema wanazo Ofisi za Uthibiti ubora wa shule ambazo zipo za Kanda na Wilaya,Vyuo 35 vya ualimu vya Serikali ambavyo vinatoa cheti na Diploma.
Amesema katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano na sita wameboresha miundombinu katika Vyuo vikuu na vyuo mbalimbali akitolea mfano Vyuo vya Maendeleo ambavyo vilikuwa na hali mbaya na udahili ulikuwa chini.
Amesema wameweza kuvikarabati vyuo vyote 54 vya Maendeleo ya Wananchi kiasi kwamba udahili umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
“Pia tumekarabati na kujenga katika vyuo vyote 35 vya ualimu na vingine ukarabati unaendelea kwenye udhibiti ubora tunazo kanda 14 kufikia mwaka mwaka 2020 tulikuwa tumejenga ofisi mpya uthibiti ubora wa shule katika Halmashauri za 100.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema mwaka 2020-2021 wamejenga ofisi 55 na kukarabati ofisi 31 yote hiyo ni katika kuongeza ubora wa elimu ambapo amesema ubora wa elimu unaendana na miundombinu bora.
SERIKALI YATOA BILIONI 1.1 KWA AJILI YA UKARABATI MAKTABA SABA
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Maktaba Taifa, Mboni Ruzegea ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kuweza kutoa zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa maktaba saba nchini.
Amezitaja Maktaba zilizofanyiwa ukarabati ni za Mikoa ya Iringa, Bukoba, Rukwa l, Kilimanjaro, Tabora, Kigoma na Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu huyo amesema mpango wa Mkakati wa Bodi ya Maktaba nchini ni pamoja na kushughulikia ramani za majengo katika sehemu ambazo hakuna huduma za maktaba.
Amesema wamepangiwa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya Maktaba mtandao kwa Maktaba zote ambazo zipo 43 na 22 za Mikoa na 19 ni za Wilaya.
Amesema changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na kupokea fedha pungufu, kutokuunganishwa katika mkongo wa Taifa.
Kwa upande wake mwanachama wa Maktaba ya mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mtumishi wa Halmashauri ya Kilolo Juma Kimenya amesema baada ya ukarabati huo wamenufaika kwani kwa sasa hali ya hewa ni nzuri kutokana na madirisha kuwa mengi.
WAELIMISHWE UMUHIMU WA KUJISOMEA
Kuhusina na utaratibu wa watanzania kujisomea, Kimenya amesema sio kila mtu anapenda kusoma hivyo kuna haja ya kuelimishana ili watu wajue umuhimu wa kusoma.
“Kujisomea hili suala kidogo unajua ni ‘altitude’ ya mtu pia na ‘traditional’ kwa sababu sio kila mtu anapenda kusoma inategemea na mtu anataka kusoma agundue nini labda tungekuwa na uwanja wa kuelimishana kuhusiana na namna ya kusoma watu wagekuja kusoma kwa sababu sio lazima usome kile ambacho umefundishwa inategemea unahitaji nini tungekuwa na uwanja wa kuelimishana,” amesema
Kwa upande wake mwanachama wa Maktaba hiyo ambaye ni mwalimu, Shida Mgaya amesema kutokana na ukatabati na maboresho hayo idadi ya wanachama imeongezeka ambapo ameomba vitabu vya kisasa viongezwe.
“Kwa sasa wanachama wameongezeka kutokana na maboresho ambayo yamefanyika madirisha meza viti na wameongeza Internet tunaomba waendelee kuongeza vitabu vya kisasa.Mwitikio sio mkubwa kwa wanaojiunga na tuendelee kutangaza kuhusu huduma za maktaba watu walikuwa hawaji lakini kwa sasa wanakuja,” amesema.
Social Plugin