Video hiyo imeibuka kwenye mitandao ya kijamii ambapo bikizee anaonyeshwa akipodolewa na kugeuka binti mchanga .
Wanamtandao wengine walihoji kuwa vipodozi hivyo vilipita kiasi
Katika video hiyo, iliyopakiwa kwenye Instagram na @arewafamilyweddings, bibi huyo anaonyeshwa akiwa ameketi huku msanii mpodoaji akimfanyia miujiza usoni.
Akipakia video hiyo, @arewafamilyweddings alisema:
"Mtashtuka kuona urembo huu baada ya kupakwa makeup"
Wanamtandao maoni Wanamtandao walijaa kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko ya bibi huyo.
Baadhi ya wanamtandao walidai kuwa bado bibi huyo angali mrembo bila kujipodoa.
Msanii mpodoaji awafurahisha wengi kwa kumbadilisha bibi wa miaka 75 iliripotia awali kuwa msanii mpodoaji Priscilla Appiah, alimiminiwa sifa mtandaoni kwa kazi yake njema.
Msanii huyo mpodoaji alimbadilisha mama yake kuwa sweet 16 na kupachika picha hiyo kwenye Instagram akimtakia heri njema akitimiza umri wa miaka 75.
Katika karne ya sasa, wasanii wapodoaji barani Afrika wamekuwa wakionyesha ubunifu wao, na kufanya miujiza.
Iwapo picha zote mbili hazitalinganishwa, watu wengi watadhania kuwa ni watu wawili tofauti katika picha moja.
Hii ndio sababu msanii huyo mpodoaji alibadilisha muonekano wa mama yake kabisa.
Akizungumza katika mahojiano, msanii huyo alisema kazi hiyo ilimchukua muda wa saa moja kukamilisha.
Social Plugin