Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGODI WA BUCKREEF WATENGA MILIONI 321 KUSAIDIA JAMII


Meneja rasilimali watu mgodi wa Buckreef Amelda Msuya akitoa maelezo kwa mbunge wa jimbo la Geita Mjni Costantine Kanyasu aliyevaa koti
Meneja wa Benki NBC tawila Geita Hilda Bwimba akitoa maelezo kwa mbuge wa jimbo la Geita Mjini Costantine Kanyasu alipotembelea kwenye banda hilo

***
Na Alphonce Kabilondo Geita

Mgodi wa Buckreef uliopo katika kijiji cha Mnekezi kata ya Kaseme Wilayani Geita umetenga zaidi ya shilingi milioni 321 ambazo ni fedha za uwajibikaji wa kampuni katika jamii (CSR) kwa kipindi cha mwaka 2021/2022.

Meneja rasilimali watu wa Mgodi huo Amelda Msuya amebainisha hayo wakati Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Costantine John Kanyasu alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye uwanja wa maonesho ya EPZ mjini Geita .

Meneja huyo amesema kuwa Mgodi huo una ubia kati ya serikali na mwekezaji TANZAM 2006 ambapo serikali inachukua asilimia 45 na mwekezaji huyo asilimia 55 hivyo kutokana na mgodi kutambua na kuthamini jamii inayowazunguka mgodi huo umetenga fedha hiyo kwa ajili wa uwajibikaji katika jamii.

Alisema mbali na kutenga fedha hiyo Mgodi huo umetumia zaidi ya shiligi milioni 32 kutoa msaada wa madawati na kukarabati miundombinu ya elimu katika shule za Tembo ,Kaseme Mkoani humo.

"Lengo la Mgodi ni kuhakikisha uchumi wa Mkoa wa Geita unapaa na jamii kunufaika na uwepo mgodi wetu"  ,alisema Meneja Msuya .

Mbunge Kanyasu akiwa katika banda la Tume ya Madini alihoji uchelewaji wa leseni za uchimbaji madini ambapo mtalaamu tume ya madini Achar Kashakar alisema tume ya madini imeboresha mfumo wa utoaji leseni za uchimbaji ambapo waombaji kwa sasa wanaomba na kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

Mbunge huyo mara baada ya kutembelea mabanda katika uwanja huo alisema maonesho hayo yameonyesha sura ya kitaifa na hivyo kuwataka wachimbaji kujitokeza katika maonesho hayo ili kwenda kujifunza namna ya uchimbaji madini wa kisasa .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com