Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA YATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA USHETU NA KATA YA NDEMBEZI MANISPAA YA SHINYANGA

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga,Emmanuel Ntobi

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MKOA WA SHINYANGA.

TAARIFA KWA UMMA.

YAH: KUTOKUSHIRIKI  UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KATIKA JIMBO LA USHETU - SHINYANGA NA KATA YA NDEMBEZI -MANISPAA YA SHINYANGA.

Ndugu Wanahabari na Watanzania.

Tunapenda kuwajulisha kuwa, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Shinyanga, hakitashiriki katika chaguzi  ndogo za marudio, ambao zimetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kufanyika Mwezi Oktoba, 2021 katika Jimbo la Ushetu, lakini pia  katika Kata ya Ndembezi Halmashuri ya  Manispaa ya Shinyanga.  Mkoa wa Shinyanga.

Kwamba, Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga, limejadili na kukubalina kutekeleza azimio la Chama la kutokushiriki Uchaguzi wowote wa marudio mpaka tutakapopata Tume Huru ya Uchaguzi nchini.

Kwa mantiki hiyo, hakuna mchakato wowote wa ndani ya chama uliofanyika, unaofanyika ama utakaofanyika unaohusu chaguzi ndogo (Utoaji fomu,kura za maoni na uteuzi) kwa kata hiyo na jimbo hilo kama ambavyo katiba ya chama ya mwaka 2006,toleo la 2019 ibara za 7.3.9(a), 7.4.10(a), 7.4.10(r) na 7.7.16(p) zinavyotaka.

Aidha, tunawasihi wanachama wetu kuendelea  kuelimishana kuhusu madai ya Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi na kuendelea kujisajili kidijitali na kutumia Chadema dijitali kwani kesho yetu ni nzuri kuliko jana.

Pamoja na Salamu za Chama

Imetolewa leo 14.09.2021 na;

Emmanuel Ntobi

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com