Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC SENGATI AFUNGUA RASMI UTEKELEZAJI WA MPANGO SHIRIKISHI NA HARAKISHI WA CHANJO DHIDI YA UVIKO-19 SHINYANGA...AAGIZA WANAOPOTOSHA WASHUGHULIKIWE

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akifungua Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr. Philemon Sengati amewaagiza wakuu wa wilaya kumshughulikia mtu yeyote atakayepotosha kuhusu chanjo ya UVIKO-19 ndani ya Wilaya za Mkoa wa Shinyanga kwani mtu huyo hautakii Mkoa maendeleo huku akitoa siku 20 kutekeleza mpango shirikishi na harakishi kuhusu utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Dkt. Philemon Sengati ametoa agizo hilo leo Septemba 27,2021 wakati akifungua kikao kwa ajili ya Mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi mkoa wa Shinyanga (PHC) ya utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kuhusu utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Kikao hicho kimekutanisha wadau mbalimbali wa afya kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya chanjo ya UVIKO-19 na namna ya kufanya uhamasishaji kwa jamii kuhakikisha walengwa wengi kwa chanjo wanafikiwa na hatimaye kupunguza maambukizi na kukinga dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

“Mtu yeyote atakayepotosha kuhusu chanjo ya UVIKO-19 ndani ya Wilaya za Mkoa wa Shinyanga basi Wakuu wa Wilaya mumshughulikie mtu huyo kwani hautakii Mkoa maendeleo”,amesema Dkt. Sengati.

Dkt. Sengati amesema kutokana na muitikio mdogo serikali imekuja na mpango mkakati unaoitwa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ili kufikia malengo ya asilimia 100 ya chanjo zote zilizopokelwa zitolewe kwa wananchi ndani ya siku 20 tulizojiwekea kama Mkoa kuanzia tarehe 01 Oktoba, 2021 hivyo hatapenda kuona mtu yeyote anapotosha kuhusu chanjo.

“Tunapofanya ufunguzi rasmi wa utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 naomba Chanjo iwe kipaumbele kwa kila mmoja wetu hivyo Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya na viongozi mbalimbali na wadau wote mshiriki na kusimamia zoezi hili na kuhakikisha kila mwananchi mwenye umri kuanzia miaka 18 anahamasika na kupatiwa chanjo”,amesema Dkt. Sengati.

Amewashauri viongozi kuwa mstari wa mbele kujitokeza kuchanja na kuhamasisha wananchi kuchanja ili wananchi waendelee kuwa imara zaidi akibainisha kuwa kuanzia kesho atafanya ziara kwenda kwenye maeneo ya kimkakati ili kuondoa mitazamo hasi kuhusu chanjo ya UVIKO - 19.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kalidushi Charles amesema wameamua kuja mkoani Shinyanga kuja kuongeza nguvu katika utoaji chanjo kwani mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 10 ya mwisho kwa idadi ya watu waliochanjwa hadi kufikia Septemba 25,2021. Mingine ni Lindi, Singida,Geita, Manyara, Rukwa, Simiyu, Njombe, Katavi na Songwe.

Amezitaja fursa zilizopo kwa ajili ya chanjo maeneo yanayotakiwa kupelekewa chanjo kuwa ni machimbo,masoko, stendi za mabasi,nyumba za ibada, viwanda, vikao na makongamano mbalimbali, taasisi mbalimbali za umme na za binafsi, vyama vya siasa, vijiwe vya bodaboda,majeshi, watoa huduma za asili na watu maarufu.

Amewaomba viongozi wa dini wahamasishe kwenye makanisa na misikiti ili waumini wao waweze kupata chanjo na waruhusu wahudumu kwenda kutoa huduma za ibada.

“Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa wilaya wanapokuwa kwenye maeneo ya wananchi kwa shughuli mbalimbali waongelee habari ya chanjo na waambatane na wahudumu wa afya wakiwa na chanjo. Pia wakuu wa wilaya wawaelekeze watendaji walio chini yao kushiriki kikamilifu katika zoezi la uhamasishaji na uchanjaji”,amesema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema zoezi la uchanjaji Chanjo ya UVIKO -19 lilianza Agosti 4,2021 na hadi kufikia Septemba 26,2021 jumla yaa chanjo zilizotumika ni 6,990 sawa na asilimia 28 ya chanjo zote 25,000 zilizotolewa mkoani Shinyanga ambapo jumla ya watu waliopata chanjo ni 6,027.

“Jumla ya watu waliopata chanjo hadi kufikia Septemba 26,2021 katika Manispaa ya Shinyanga ni 2445, Manispaa ya Kahama 1863, Halmashauri ya Kishapu 651, Msalala 640, Shinyanga 312 na Ushetu 116”,ameeleza Dkt. Ndungile.

“Katika siku 54 za utoaji chanjo Wanaume wameongoza kuchanja chanjo ambapo jumla ya wanaume 4015, Wanawake ni 2012 hivyo kuna umuhimu wa kuhamasisha wanawake kujitokeza kuchanja",amesema.

Amesema zoezi la utoaji vyeti vya Kielektroniki kwa watu waliochanjwa chanjo ya UVIKO – 19 linaendelea vizuri.

Nao Wadau wa afya walioshiriki kwenye kikao hicho wamesema "Chanjo ni muhimu sana kwa mustakabali wa kiuchumi wa taifa na unapochanjwa unakuwa imara,utakuwa na nguvu ya kuhimili ugonjwa huo ili uweze kuendelea kutekeleza majukumu yako".

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akifungua Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19 leo Jumatatu Septemba 27,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akifungua Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19 leo Jumatatu Septemba 27,2021
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kalidushi Charles akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kalidushi Charles akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19

Mratibu wa Chanjo ya UVIKO - 19, Timoth Sosoma akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19

Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga , Chillah Moses na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile wakiwa kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kalidushi Charles (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati wakiwa kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akifunga Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19
Picha za kumbukumbu wadau mbalimbali wa afya baada ya Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19.
Picha za kumbukumbu wadau mbalimbali wa afya baada ya Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Mkoa wa Shinyanga kinachohusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com