MTANDAO WA MISITU AFRIKA 'AFF' WAFANYA MKUTANO WA KUBADILISHANA UZOEFU


Kaimu Mkuu wa chuo SUA Profesa Raphael Chibunda

Mtandao wa Misitu Afrika – AFF umefanya mkutano wa kubadilishana uzoefu kuhusu utekelezaji wa mkataba Paris uliotaka kuimarishwa kwa usimamizi wa misitu ili kupunguza madhara yaletwayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao na kushirikisha nchi nne za Afrika umefunguliwa rasmi na Kaimu mkuu wa chuo kikuu cha Kilimo cha SOKOINE – SUA Profesa Raphael Chibunda katika hotuba yake iliyosomwa na Profesa Esron Karimuribo wa SUA.

Katika hotuba yake Profesa Chibunda amepongeza waandaaji wa mkutano huo kwa kuweza kutumia teknolojia ambayo imewezesha washiriki zaidi ya 200 kukutana na kujadili kuhusu masuala ya misitu na biasahara ya utomvu (gum) ambayo ni zao majawapo la misitu.

Profesa Chibunda amesema majadiliano ya kubadilisha uzoefu na maarifa kuhusu masuala ya misitu ni njia sahaihi ya kuobersha hatua za kukabiliana na adhari za mabadiliko ya tabianchi na hatimaye na kuboresha Maisha ya jamii zinazomiliki misitu hiyo.

Kundi la washiriki wa Tanzania lilikutana katika kituo cha kitaifa cha kufuatilia hewa ukaa – NCMC katika katika chuo kikuu cha Kilimo cha SOKOINE – SUA mkoani MOROGORO.

Nchi zilizoungana na kundi la Tanzania ni Gambia, Botswana na Kenya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post