Na Fabian Fanuel, Mwanza.
Mashindano ya Angeline Jimbo Cup 2021 yamemalizika mwishoni mwa wiki huku timu ya kata ya Kirumba ikiibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya kata ya Ibungilo kwa penalti 4-3 baada ya kutoka sare 1-1 ndani ya dakika tisini.
Katika michuano hiyo ambayo imeanzisha na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Kwa ushirikiano wa Taasisi ya The Angeline Foundation, hatua kubwa imeonekana toka michuano ya msimu wa kwanza hadi ya juzi Ikiwa ni msimu wa tatu.
Pamoja na ukomavu wa mashindano hayo ila ushindani umeongezeka kutoka timu mbalimbali ambazo huwa zinapatikana katika Kila Kata ambazo ziko kwenye Jimbo la Ilemela ambalo Mbunge wake ni Mheshimiwa Dkt Angeline Mabula.
Kwa msimu mitatu ya mashindano hayo, yameongezeka hamasa, ubunifu na hadhi ya mashindano inazidi kukua siku hadi siku. Kiwango cha mashindano kinazidi kuboreka kutokana na kamati ya maandalizi na wasimamizi wa michuano hiyo.
Moja Kati ya eneo liliboreshwa ni kwenye zawadi, Zawadi zimeboreshwa na kuongezewa thamani. mshindi akipita milioni mbili, wa pili milioni moja na nusu na watatu akipata milioni moja. Huku zawadi zingine kama kipa bora, mwamuzi bora, Mchezaji Bora, Kikundi bora cha ushangiliaji na Mwandishi Bora zikiongezewa thamani.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ufungaji wa Mashindano hayo, aliyekuwa Mgeni rasmi Jamal Babu ambaye ni mjumbe wa halmashauri ya Taifa CCM, alisema michuano hiyo imeibua vipaji vingi ambayo tayari timu mbalimbali hapa Tanzania zimeanza mazungumzo kuwasajili.
"Angeline Jimbo Cup 2021, yamekuwa Mashindano makubwa Sana. Vipaji vingi vimeonekana na vimepata nafasi ya Kucheza. Tegemea kuona Fursa kubwa kwa wachezaji mbalimbali waliohusika kutoka timu zote na hii ndio Fursa ya nafasi ya kusajiliwa" alisema Jamal Babu.
Kwa upande wake Mwasisi na Mmiliki wa Mashindano hayo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula alisema kuwa wamefarijika michuano kuwa mizuri na imeleta hamasa kubwa Jimbo humo na watazidi kuiboresha Kila Mwaka.
"Michuano ya Msimu huu imekuwa mikubwa Sana. Mwanzoni tuliona hamasa ila kadri siku zilivyokwenda ndio hamasa iliongezeka Sana. Kikubwa niwashukuru wote waandaji, wasimamizi wa Viongozi wa timu zote na Wachezaji Kwa kuwajibika kikamilifu. Hakika Mmetupa deni la kuzidi kuboresha Mashindano Haya mwakani" alisema Dkt Mabula.
Michuano ya Angelina Jimbo Cup 2021 imeshirikisha timu 19 za kutoka Kata mbalimbali za Jimbo la Ilemela. Pamoja na Timu za mpira wa miguu Kwa wanaume ila pia mwaka huu Mashindano mengine kama Mpira wa miguu Kwa wanawake yamekuwepo na mashindano aina mbalimbali ambayo yameleta hamasa kubwa.