Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Timu ya Geita Gold FC inatarajia kutumia uwanja wa CCM Kambarage kama uwanja wa nyumbani Ligi Kuu Soka Tanzania bara msimu wa 2021/2022 ambapo kesho Septemba 2, 2021 itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Shinyanga Combine.
Akizungumza na Malunde 1 blog, Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga, Said Mankiligo amesema tayari Kocha Mkuu Ndairagije aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Star na Msaidizi wake Fred Felix Minziro na kikosi chote cha timu wameshawasili Mjini Shinyanga.
“Timu ya Geita Gold Football Club imechagua uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kuwa uwanja wa nyumbani kwa kipindi hiki ambacho wanaendelea na matengenezo ya uwanja wao”,amesema Mankiligo.
“Timu ya Geita imewasili Shinyanga tangu Agosti 31,2021 na leo wameanza rasmi mazoezi yao na kesho Alhamis saa 10 jioni watacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Shinyanga Combine (inayojumuisha Mastaa wote Shinyanga) katika uwanja wa CCM Kambarage”,ameongeza Mankiligo.
Amesema pia Timu ya Geita Gold FC inatarajia kucheza michezo ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre Season) na timu za Police Tanzania na Biashara United ya mkoani Mara ambapo ratiba ya michezo itatangazwa kesho.
Social Plugin