Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watangazaji wa Vipindi vya Redio na Televisheni wametakiwa kuwa wabunifu zaidi na kujituma kuhakikisha kwamba leseni ya utangazaji iliyotolewa na TCRA wanaitendea haki kwa nia ya kuwawezesha watanzania kuhabarishwa kwa ubunifu zaidi.
Rai hiyo imetolewa Septemba 3,2021 na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo Mjini Kahama wakati wa uzinduzi Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz chenye kauli mbiu ya 'Sauti ya dhahabu' ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa.
Mhandisi Mihayo aliwataka watangazaji na waandishi wa habari kuwa wabunifu zaidi ili kuitendea haki leseni ya utangazaji inayotolewa na mamlaka hiyo kwa nia ya kuwawezesha Watanzania kuhabarishwa kwa ubunifu zaidi.
“Gold Fm walianza vizuri sana na wameanza kufanya kazi vizuri sana. “Kwa kweli wameanza vizuri ndiyo naomba mjiandae kufungua Kituo cha Televisheni itakayotangaza kutoka Kahama. TCRA tuna utaratibu wetu wa kuhakikisha Leseni yetu inafuatwa. Naomba niseme tu, tulipowapa leseni tulileta wataalamu kwa ajili kufuatilia mwenendo wa matangazo ya Gold Fm bila wao wenyewe kujua, kuna mahali waliteleza niliwapigia simu na wakaniahidi kuwa hawatarudia”,alisema Mhandisi Mihayo.
“Gold Fm tumewapa leseni, ile leseni kule nyuma kuna maelekezo, sasa maelekezo hayo nawaomba kama hamuyaelewi, ofisi yangu ya Kanda ipo wazi masaa 24 kwa ajili ya kukusaidia na kukuelekeza, usije ukafanya kosa ukifikiri kuwa hatutafuata sharia,sisi tutaendelea kufuata sheria na taratibu zilizopo”,aliongeza.
“Kwa hiyo nategemea jinsi mlivyoanza vizuri namna hii, muongeze usikivu kama tulivyotoa kibali sasa hivi kwa mkoa mzima wa Shinyanga lakini siyo kuongeza usikivu tu lakini muende kwa mwendo wa kisasa. Nawapongeza mpo kwenye mtandao,popote duniani mnasikika. Lakini muongeze ubunifu,muongeze kujituma ili kuhakikisha kwamba ile leseni iliyotolewa na TCRA mnaitendea haki”,alisema Mhandisi Mihayo.
Aidha Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa alisema amekubali ombi la Mkurugenzi wa Gold FM, Bi. Neema Mghen kuhusu Gold Fm kuongezewa maeneo ya usikivu akipenda Redio hiyo isikike katika mkoa wote wa Shinyanga.
“Mkurugenzi wa Gold Fm ametoka hapa akisema anaomba kibali cha kusikika mkoa mzima wa Shinyanga. Mhe. Mgeni Rasmi naomba niseme kibali kimetolewa kuanzia sasa. Gold Fm njooni tuzungumze, nitawaelekeza jinsi ya kufanya ili muweze kusikika mkoa mzima wa Shinyanga”,alisema Mhandisi Mihayo.
“Mhe. Mgeni rasmi tunahitaji sana katika Kanda ya Ziwa tuwe na usikivu wa Redio kila wilaya kwa sababu kwa sasa tupo chini ya asilimia 50. Ninapozungumza leo mimi nina furaha kuanza kwa Gold Fm kwa sababu tunaenda kufikisha Redio 39 Kanda ya Ziwa na kwa upande wa Shinyanga sasa Gold Fm inakuwa Redio ya tano”,alieleza Mhandisi Mihayo.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amepongeza uwekezaji mkubwa wa Gold Fm na wa kisasa uliofanyika ambao utaenda sanjari na upatikanaji wa ajira.
“Ninafurahi kuona uwekezaji wa namna hii unaenda sehemu husika (Kahama), na endapo mtahitaji kuanzisha television nawashauri mkiweza anzeni mapema na mkihitaji msaada tuambieni hiyo ndiyo kazi yetu”,alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo cha Gold FM Bi. Neema Mghen ameiomba Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa kushirikiana na Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuvijengea mazingira wezeshi vituo vichanga vya redio ili viendelee kuwa daraja la kuwasaidia wasanii wachanga kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa kituo cha Gold FM Bi. Neema Mghen akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na wafanyakazi wa Gold Fm.
Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Zoezi la Uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm likiendelea
Zoezi la Uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm likiendelea
Muonekano wa sehemu ya Jengo la Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akisaini Kitabu cha Wageni wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), Emmanuel Cherehani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akiingia katika chumba cha habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (wa pili kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga, Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ( wa kwanza kulia akifuatiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen (wa pili kulia) wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga (kulia) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ndani ya chumba cha kutengenezea vipindi (Production Room)
Mtangazaji wa Vipindi vya Redio, Juma Athuman (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (aliyekaa kulia) ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'. Wa Kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo, Kushoto aliyekaa ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga, aliyesimama mwenye suti ya bluu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Mtangazaji wa Vipindi vya Redio, Juma Diwani (kulia) akimuuliza swali Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) wakati akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia :
Social Plugin