Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TGNP YAMPONGEZA DKT. ASHATU KACHWAMBA KIJAJI KWA KUTEULIWA KUWA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

PONGEZI KWA DKT. ASHATU KACHWAMBA KIJAJI KWA KUTEULIWA KUWA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI. 


Kwa niaba ya wanachama, bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi/watumishi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), tunayofuraha kumpongeza Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na hivyo kutengeneza kestoria ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kushika nafasi hiyo. Hatua hii ni kubwa sana katika historia ya harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi nchini na Afrika kwa ujumla.  


Dkt. Kijaji alikuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Fedha na Mipango kuanzia mwaka 2015-2020.


Ni matarajio yetu na watanzania kwa ujumla kuwa kutokana na uzoefu katika uongozi, Dkt. Kijaji katika nafasi yake ya Uwaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ataendelea kusimamia uzalendo na kutetea wanyonge hasa wanawake na makundi yaliyopembezoni dhidi ya dhuluma za kijinsia wanazokutana nazo katika sekta hiyo ya habari, mawasiliano na teknolojia ili kuleta maendeleo endelevu na jumuishi yenye kuzingatia usawa wa kijinsia.  




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com