Msanii wa Bongo Movies, Jacob Steven maarufu kama JB ametangaza kuachana na kazi ya uigizaji na kujikita zaidi katika uongozaji na uandaaji wa filamu.
JB ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram;- ‘’Niliwahi kusema napumzika kufanya filamu na nitabaki kwenye tamthilia.. lakini sasa Nafikiria kupumzika pia kuigiza na nitabakia nyuma ya camera kama Producer na Director.
Tamthilia yangu ya #mwanamuzikiseries nafikiri itakuwa ndio ya mwisho..kuigiza.. Ni matumaini yangu kwenye kipindi chote. Tangu 1997 wakati naanza mambo hayo mpaka 2000 wakati naanzisha Jerusalem films umefurahia kazi zangu..lakini nakuahidi huo ni mwanzo tu..mengi mazuri yanakuja nikiwa nyuma ya camera.’’
Social Plugin