Wananchi wakiwa kwenye kaburi hilo
Hali ya taharuki imetokea katika kitongoji cha Kipondoda wilayani Manyoni mkoani Singida, baada ya mwili wa marehemu Julia Amasi mwenye umri wa miaka 93 kuzikwa hapo jana na asubuhi ya leo kukuta kaburi likiwa limefukuliwa likiwa na jeneza pekee huku mwili ukiwa pembezoni mwa makaburi hayo.
Mara baada ya kukuta kaburi hilo likiwa hakuna mwili wa marehemu ndipo wakaanza kutafuta na kuukuta mwili ukiwa kando kidogo ya makaburi hayo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kipondoda Jackson Job amelaani tukio hilo kwa kuwa vitendo hivyo vya uchimbuaji makaburi baada ya kuzika vimezidi kukithiri katika mji wa Manyoni.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Manyoni Amina Mohammed ametoa wito kwa wananchi kuwafichua wale ambao hawatambuliki wakiwemo waganga wa kienyeji ambao ndiyo wanasadikika kuwa chanzo cha kutokea vitendo hivyo.
Social Plugin