KATAMBI ATOA MSAADA VIFAA SAIDIZI KWA WATU WENYE ULEMAVU SHINYANGA



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye suti katikati, akikabidhi baiskeli za magurudumu matatu, kwa watu wenye ulemavu, kulia kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Sigara TCC Amani Lyimo, na kulia ni Katibu wa Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Migeyo Ally.


Na Marco Maduhu, Shinyanga
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, Patrobas Katambi, amekabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu Manispaa ya Shinyanga.

Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, amekabidhi vifaa hivyo leo, zoezi lililofanyika kwenye Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Alisema katika kipindi cha Kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka 2020 aliahidi kutatua changamoto mbalimbali za watu wenye ulemavu, na kuamua kuanza kuwapatia msaada wa vifaa saidizi.

"Vifaa saidizi ambavyo navitoa kwa watu hawa wenye ulemavu, ni Baiskeli 10 za magurudumu matatu, fimbo nyeupe 60, pamoja na magongo pea 60," alisema Katambi.

Aidha, alisema Serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali za watu wenye ulemavu, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuwapatia mikopo ya Halmashauri asilimia 2, ili wajikwamue kiuchumi.

Katika hatua nyingine Katambi, aliipongeza Kampuni ya Sigara TCC, kwa kukubali ombi lake, na kuamua kumpatia vifaa hivyo saidizi, kwa ajili ya kuwapatia watu hao wenye ulemavu.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu mkoani Shinyanga (SHIVYAWATA) Mohamed Ally, alimpongeza Katambi kwa msaada wa vifaa hivyo saidizi, kuwa vitawasaidia kufika maeneo mbalimbali, wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akizungumza kwenye zoezi hilo la kukabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akizungumza kwenye zoezi hilo la kukabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu na kuahidi kuwa Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kutatua changamoto zao.

Meneja Kampuni ya Sigara Kanda ya Sinyanga, Tabora, na Meatu, Amani Lyimo, akizungumza kwenye zoezi hilo la ugawaji vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye suti katikati, akikabidhi Baiskeli ya Magurudumu Matatu, kwa watu wenye ulemavu, kulia kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Sigara TCC Amani Lyimo, na kulia ni Katibu wa wazazi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Migeyo Ally.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye suti katikati, akikabidhi Baiskeli ya Magurudumu Matatu, kwa Happyness Kasembo, kulia ni Meneja wa Kampuni ya Sigara TCC Amani Lyimo, kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune.

Katambi akiendelea na zoezi la ugawaji Fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu.

Zoezi la ugawaji vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu likiendelea.

Zoezi la ugawaji vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu likiendelea.

Zoezi la ugawaji vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu likiendelea.

Zoezi la ugawaji vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu likiendelea.

Katambi akipiga picha ya pamoja na watu wenye ulemavu, wakiwamo viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Na Marco Maduhu-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post