Mfanyabiashara wa duka la simu mkoani Katavi amemfumania rafiki yake ambaye ni mfanyabiashara wa zao la mpunga katika Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele mkoani humo kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na mke wake wakihondomolana (wakivunja amri ya sita).
Taarifa zimeeleza kuwa baada ya jamaa huyo kufumaniwa, rafiki yake huyo alimtaka kumlipa faini ya pesa kiasi cha shilingi milioni 5, kiasi ambacho alikilipa bila pingamizi yoyote.
Kupitia mitandao ya kijamii kuna video inasambaa ikimuonesha jamaa alivyofumaniwa, na akisikika rafiki yake akizungumza kwa uchungu, kuhusu rafiki yake huyo kujihusisha kimapenzi na mke wake ambaye wamezaa mtoto mmoja.
Social Plugin