Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Ulrich Matei
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuwatorosha watoto 11 wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 14, kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya na kwenda kuwauza kwa wafugaji.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Ulrich Matei, na kusema kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakiwauza watoto hao kwa gharama ya kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000, kwa wafugaji wilayani Mbarali ili wachunge mifugo yao.
Mbali na hili Jeshi la Polisi pia linawashikilia walimu wawili kwa tuhuma za kutaka kuharibu mitihani ya mwisho ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi.
CHANZO - EATV
Social Plugin