Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kwenye moja ya mabanda baada ya kuwasili katika viwanja vya EPZA kwenye maonesho ya nne ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili katika viwanja vya EPZA kwenye maonesho ya nne ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye maonesho ya nne ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita
***
Na Alphonce Kabilondo,Geita
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za fedha nchini kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwakopesha mikopo yenye masharti nafuu au vifaa vya uchimbaji wa madini.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akifungua rasmi Maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye sekta ya madini kwenye eneo la uwekezaji kiuchumi EPZA Mkoani Geita huku akisema kuwa sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi na kuchangia kwenye pato la Taifa.
Amesema taasisi za kifedha zimepewa dhamana ya kufanya shughuli zao na zinapaswa kuwasaidia wachimbaji kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu au vifaa,mitambo ya uchimbaji ili waondokane na kutumia dhana duni ili wachimbaji waweze kufanikiwa na kuleta tija.
"Benki ya Taifa ya Biashara pamoja na taasisi zingine za kifedha zimeanza kuwa kopesha wachimbaji taasisi za fedha wakopesheni fedha wachimbaji mikopo ya mashariti au vifaa vya uchimbaji na mitambo waachane na kutumia dhana duni", alisema Wazairi Mkuu.
Aidha mkrugenzi kitengo cha biashara kutoka benki ya taifa ya biashara NBC Elvis Ndunguru alisema kuwa Benki hiyo imeanza kutoa mikopo kwa vikundio vya wachimbaji mtu mmoja mmoja pamoja na watoa huduma migodini.
"Tumeanza utaratibu kuwapatia elimu wachimbaji wadogo na kuwakopesha kwa vikundi wachimbaji wadogo kwa vikundi vya wachimbaji pamoja na mtu mmoja mmoja na baadae kuwakopesha mitambo kwa kutumia leseni zao kama dhamana", alisema Elvis.
Makamu wa Rais wa migodi ya Ashanti Saimon Shayo akizungumzia mchango wa sekta ya madini mkoani humo alisema kuwa kipindi cha miaka mitatu mgodi wa GGML umechangia zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa lengo la kusaidia jamii katika shughuli za maendeleo.
Rais wa shirikisho la wachimbaji wadogo nchini FEMETA Bw. John Bina akitoa salaamu za wachimbji wadogo alisema kuwa wachimbaji wataendelea kulipa kodi za serikali huku akiiomba serikali kuweka msukumo kwenye taasisi za kifedha ziweze kuwakopesha mikopo ya masharti nafuu .