Naibu Waziri wa Madini Profesa Shukrani Manya akiongea na wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Matongo katika kata ya Ikungi wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Kamishina wa Madini Nchini Dkt. Abdulrahman Mwanga akiwaeleza wachimbaji hao namna tume ya madini inavyo fanya kazi zake.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akiongea na wachimbaji hao wa Matongo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Na Edina Malekela,Singida.
Naibu waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya amewataka wachimbaji wadogo wa Madini kuacha kuzalisha migogoro isiyo ya lazima badala yake watumie fursa hiyo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Prof. Manya alitoa agizo hilo jana wakati wa kikao chake na wachimbaji wadogo wa Mgodi wa dhahabu uliopo katika kijiji cha Matongo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida huku akiwataka wachimbaji hao kufanya kazi kwa kupendana na katika hali ya usalama ili kuepusha migogoro.
"Serikali imeelekeza maeneo yote ya uchimbaji yanapaswa kuchimbwa kwa usalama lakini pia kwa kupendana jambo hilo mlishike sio kama mimi ni Mchungaji nawahubiria hapa lakini mkiondoa upendo katika shughuli zenu nyinyi kila siku mtakuwa mnataka migogoro na mtafanya Wizara ya Madini ionekane ni wizara ya migogoro kumbe ni Wizara ya kutoa huduma kwa wachimbaji ili kuleta tija kwa maisha yenu binafsi na maendeleo ya uchumi wa Taifa letu", alisema Manya.
Akitolea ufafanuzi juu ya mgogoro kati ya Mama Helena Robati Mtaturu na Richard Lymuya uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja alisema mgogoro huo ni kuchanganya mambo mawili kati ya mmiliki wa leseni na mmiliki wa shamba na kwa jinsi hiyo kukazalishwa mgogoro uliotokana na kutokuwa na uelewa kwa Mama Helena Mtaturu.
"Unashamba lako kweli na unania ya kuchimba nenda ofisi ya Afisa Madini Mkazi kata leseni kabla ya kuzamisha sururu kama hujafanya hivyo Sheria ya Madini inasema kwamba muombaji yeye huyo atapewa tukijua tunampa mtu huyo kwenye shamba la mtu huko, Mwenye shamba kama sio mchimbaji watakuwa na makubaliano yao sasa ndugu zangu na Migodi mingine yote mmnayoiona walifanya hivyo ndiyo maana huoni migogoro huko." alisema Manya.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro alisema kuwa wakati wa mtangulizi wake Edward Mpogolo ofisi ilisikiliza mgogoro wa Mama Helena Mtaturu na ofisi ikaelekeza swala hilo lishughulikiwe na Kamishina msaidizi wa Madini mkoa na yakatoka makubaliano katika eneo hilo pasiendelee na uchimbaji mpaka muafaka utakapopatikana.
Alisema kwa taarifa iliyopo ofisi ya DC, Mama Helena alikiuka makubaliano ambapo aliendelea kufanya shughuli katika mgodi huo bila kusubiri kama alivyoelekezwa kutokufanya shughuli yeyote mpaka pale mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi.
"Kukamatwa na kupelekwa Polisi kwa Mama Helena haihusiani na leseni ni kukiuka makubaliano kwamba jambo hili kaa litulie na mzigo huu utulie mpaka swala litakapoisha ndiyo kazi iendelee Mama huyo akapata watu wayanja wakamshauri vibaya", alisema Muro.
Aidha aliongeza kuwa kuhusu kushinikizwa kwa Mama Helena kusaini leseni na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo sio kweli baada ya kusaini Helena alikaa kimya baada ya vurugu kuanza ndiyo akaipuka tena na kusema ameshinikizwa, lakini kwa maelezo ya mtangulizi Mpogolo yanasema Mama Helena anavishoka wanataka eneo hilo kwa shughuli ya uchimbaji.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini mkoani Singida (SIREMA) Selemani Omary wakiwa na katibu wake Hamisi Ally waliinuka na kusema kuwa Mama Helena anawatu wanaoutaka mgodi huo waliokuwa wakichimba na marehemu mume wake kipindi cha nyuma ndio wanaoutaka huku wakisema kuwa walishakaa vikao zaidi ya mara nne wakimpa elimu lakini haelewi na kusema uongo hadi kwa Waziri wa Madini kuwa ametapeliwa na kunyanyaswa wakati anapata asilimia 40 kila mzigo unapo toka na nimshirika wa shimo hilo.
Social Plugin