Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BONDIA MAARUFU MANNY PACQUIANO ATANGAZA KUSTAAFU MASUMBWI




Manny Pacquiao

Bondia maarufu Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo baada ya kuutumikia kwa miaka 26.

Pacquiao ambaye ndiye bondia pekee kutwaa ubingwa wa Dunia mara 8 katika uzani tofauti tofauti, anastaafu akiwa na umri wa miaka 42, akiwa amepigana mara 72, ameshinda mara 62, kapoteza mara 8 na sare mara 2.

Tamko lake kupitia mitandao ya kijamii linakuja ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza pambano dhidi ya Yordenis Ugas

Wiki kadhaa zilizopita, Pacquiao alitanganza kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya Urais katika Uchanguzi Mkuu wa nchini Ufilipino utakaofanyika mwakani na itajwa kuwa pia ni sababu kubwa iliyopelekea astaafu kucheza masumbwi.

''Kwenu mashabiki wakubwa na mchezo mkubwa ulimwenguni, asante! Asante kwa kumbukumbu zote nzuri. Huu ni uamuzi mgumu zaidi ambao nimewahi kufanya, lakini nina amani nao. Kimbilia ndoto zako, fanya kazi kwa bidii, na uangalie kinachotokea. Kwaheri ndondi.''ameandika Manny Pacquiao.

Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com