Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia askari watatu wa Suma JKT kwa tuhuma za kumtesa hadi kumuua mkazi wa eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Almasi Mohamed wakimtuhumu kwa wizi wa mahindi.
Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Jastine Maseju amesema watuhumiwa hao ni walinzi shamba la Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mbegu za Kilimo (ASA) lililopo eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru.
Chanzo - Mwananchi
Social Plugin