Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene
Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wake na waandishi wa habari huku akisema hali hiyo haitavumilika na kwamba kuanzia sasa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa wale wote watakao endelea na tabia hiyo.
Simbachawene amesema kila mwananchi anapaswa kusimamia matumizi sahihi ya mitandao ukiwemo wizi unaofanyika pamoja na uhuru wa kutoa mawazo ambao wengi wamekuwa wakiutumia vibaya kwenye mitandao ya kijamii.
"Namuagiza Kamishina wa polisi nchini Camillus Wambura kushughulikia wale wote wenye malalamiko ya kutoa fedha ili kesi zao zishughulikiwe na jeshi la polisi kwenye kesi za makosa ya jinai,"amesema .
Aidha Waziri Simbachawene amebainisha kwamba zaidi ya shilingi milioni 500 hadi Bilioni 1 fedha za wananchi wanyonge, wastaafu huibiwa na matapeli kwa njia ya mitandao .
"Kuna wananchi hulipishwa fedha pindi wanapoenda kulalamika kupotelewa na vitu vyao ikiwemo simu za mkononi na baadhi ya polisi kuwadai wananchi fedha ,nawaomba polisi kuacha mara moja tabia hiyo na mkasimamie haki na maadili,"amesisitiza Simbachawene.