Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 ambaye alimtukana jirani yake atalipa faini ya KSh 10,000 au atatumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani.
Emily Achieng alipatikana na hatia kisha kuhukumiwa katika mahakama ya Kibera baada ya kukiri mashtaka ya kumtusi Selina Akinyi kwa njia inayoweza kuvuruga amani.
Alitenda kosa hilo katika eneo la Katwekera lililoko mtaa wa Kibera mnamo Septemba 9, 2021 ripoti ya Nairobi News ilisema.
Mtuhumiwa anasemekana kusema maneno "nenda ukamfufue babako kutoka kaburini ili aniambie hapa alipata Ukimwi."
Mahakama iliarifiwa kwamba kabla ya kisa hicho, Akinyi ambaye alikuwa akifanya usafi alimwaga maji yenye taka karibu na nyumba zao hatua mabyo ilimuudhi Achieng.
Mabishano yaliibuka kabla ya Achieng kuanza kumrushia matusi Akinyi.
Hata hivyo, Achieng aliiambia mahakama kwamba alijibu tu matusi ambayo Akinyi alimrushia wakati wa mabishano.
Social Plugin