KINONDONI KUHAMASISHA USAFI NA UTALII KIBURUDANI ZAIDI

 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe

Na Magreth Katengu - Dar es salaam

Katika kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kutaka mkoa wa Dar es salaam kuweka mazingira safi kwenye fukwe,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameandaa tamasha la Dar Sunset Canival kwa lengo la kuweka mazingira safi na kukuza utalii.

Akizungumza na waandish wa habari, Gondwe amesema tamasha hilo kubwa litafanyika Oktoba 3 mwaka huu ,ambapo madhumuni ya tamasha hilo ni kuhamasisha wakazi wa Kinondoni kujali na kuzingatia usafi wa mazingira wakati wote.

"Juma mosi iliyopita tulianza kampeni ya kufanya usafi katika fukwe zetu kwa kuanzi fukwe ya Cocobeach mwitikio ulikuwa mzuri,tumeona baadhi ya balozi kama sita hivi zilishiriki wakiwa pamoja na wadau mbalimbali na nimatumaini yetu wadau wataendelea kujitokeza kwa wingi",amesema 

"Niwahimize Wana Kinondoni na Dar es salaam kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo, kwenye canival hiyo watapata burudani mbalimbali,kutakuwa na wasanii wa bongo flavor,vikundi vya ngoma vya utamaduni, bila kusahau michezo ya watoto na tamasha hili litakuwa endelevu", amesema Gondwe


Kwa upande wake Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni Kheri Missinga amesema Fukwe zikitumika vizuri zitakuwa kicho kikubwa cha ajira,mapato na utalii.

Naye mmoja wa wadau  Bi. Wadida Mbaraka ambaye ni meneja biashara na masoko wa kampuni ya Cocacola kwanza amesema coca-cola ipo tayari kushirikiana na serikali katika masuala yote ya maendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post