Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga
***
Jumla ya Makada saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wamechukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya udiwani wa kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga amesema wanachama 8 wa CCM waliochukua ya kuomba ridhaa kugombea udiwani kata ya Ndembezi kuwa ni Pendo Sawa, Samwel Jackson, Gelewa Njelo, Solomon Najulwa Nalinga, Dotto Joshua, Victor Thobias na Hamis Hamis (ambao pia wamerudisha fomu) na Dkt. Ezekiel Meshaki ambaye hajarudisha fomu.
Bwanga amesema mchakato wa kumpata Diwani wa kata ya Ndembezi unafuatia aliyekuwa diwani wa kata hiyo David Nkulila kufariki dunia hivi karibuni ambaye pia alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga.
“Wote waliochukua fomu hizo ni wanachama halisi wa CCM ,wanachama hai na wana sifa zote za kugombea nafasi ya uongozi. Kabla ya tarehe 25 tutakuwa tumeshapendekeza jina la mgombea mmoja ambaye anaweza kuingia moja kwa moja kwenda kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya udiwani”,ameongeza.
Social Plugin