Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwasalimia wanachama wa CCM wakati akirudisha fomu leo Jumapili Septemba 19,2021
Mgombea Udiwani Kata ya Ndembezi Mvano Abdul Idd wa chama cha ACT Wazalendo
Na Mapuli Misalaba na Amos John Shinyanga
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya udiwani katika uchaguzi mdogo kata ya Ndembezi limehitimishwa leo Jumapili Septemba 19,2021 ambapo wagombea wawili kati ya 11 waliochukua fomu wameteuliwa kuviwakilisha vyama vyao kwenye kinyang’anyiro hicho
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Ndembezi Timothy Andrew Timothy amewataja walioteuliwa kuwa ni Mvano Abdul Idd wa Chama cha ACT wazalendo na Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi CCM baada ya kukidhi matakwa ya kikanuni ya Tume ya Uchaguzi ikiwemo kuchukua na kurudisha fomu kwa wakati uliopangwa.
Afisa huyo amevitaja vyama tisa ambavyo wagombea wake hawakufanikiwa kurudisha fomu kuwa ni Abdallah Sube wa Chama cha Demokrasia Makini,Rehema Mjengi (ACD), Antony Ndida (SAU), Ramla Shija (NLD), Fatuma Ally (UMD), Emiliana Malema CCK, Ibrahim juma (CHAUMA), Lwitakubi Kabugulu (NRA), Amen Isangi (DP)
Msimamizi huyo wa uchaguzi amesema hatua inayofuata baada ya uteuzi wa majina ya wagombea ni wananchi kuweka pingamizi zoezi ambalo litahitimishwa kesho Jumatatu Septemba 20,2021 saa kumi jioni ili kuruhusu hatua nyingine za mchakato wa uchaguzi kuendelea
Aidha Timothy amesema kikao kilichowateua ni kikao cha wasimamizi wa uchaguzi ambapo ametoa wito kwa wananchi kwa yeyote mwenye pingamizi juu ya hao walioteuliwa ofisi ziko wazi ndani ya muda uliopangwa.
Mchakato huo wa uchaguzi unafuatia aliyekuwa Diwani wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga David Nkulila ambaye pia alikuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga kufariki dunia hivi karibuni.
Akirudisha fomu, Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisindikizwa na Wanachama na makada wa CCM.
Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwasalimia wanachama wa CCM akirudisha fomu leo
Social Plugin