Machimu Mshono Ndalo maarufu Ng'wana Ndalo enzi za uhai wake
Na Suzy Luhende, Shinyanga
Mazishi ya Mwili wa Mganga Maarufu wa kutoa tiba asili Machimu Mshono Ndalo almaarufu Ng'wanandalo aliyefariki dunia Septemba 20,2021 yamefanyika nyumbani kwake katika kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga Septemba 22,2021.
Marehemu Ng'wanandalo alianza kuugua tangu mwaka 2017 ambapo alikuwa akisumbuliwa na kansa ya kibofu cha mkojo kwa muda mrefu, hivyo akitibiwa na kupata nafuu lakini ilipofika tarehe 20/9/2021 majira ya saa sita usiku alifariki dunia.
Ng'wanandalo alizaliwa mwaka 1955 na alisoma shule ya msingi Imalilo mwaka 1967, alikuwa mkulima, mfugaji, mfanyabiashara na alikuwa ni Mganga wa kutoa huduma ya tiba asili na katika uhai wake alifanikiwa kuoa wake 21 ameacha wake 4 na ameacha watoto 56 wajukuu 73 na vitukuu saba.
Katibu wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salu amesema Mwanandalo alijiunga katika Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977/5/2, amekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu katika Jumuia ya Wazazi CCM Taifa na alikuwa Kiongozi mzuri wa kujitolea hivyo wameondokewa na Kiongozi Mahiri Mungu ampumzishe kwa amani.
Kwa upande wake Shemeji wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Tumaini alisema kwa sababu shemeji yake alikuwa na roho nzuri na akioa katika familia anamhudumia mke pamoja na familia ya mke wake aliwaomba wanawake walioachwa wasiolewe wamuenzi Ng'wanandalo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo Monika George na Kwangu Maige walisema marehemu alikuwa ni mtu wa kusaidia kwa yeyote atakayekuwa na shida alikuwa akimsaidia hivyo wameachiwa pengo kubwa sana.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kasim alisema wameondokewa na mtu muhimu sana katika chama kwani alikuwa ni mshauri mzuri Mungu ampokee huko aliko, kwani Mungu amempenda zaidi
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakitoka kumzika Mwanandalo
Social Plugin