Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NYUKI WAVAMIA GHAFLA MSIBANI...WAUA MZEE WA KIJIJI WAKATI WA MAZISHI

Kundi la nyuki walivuruga hafla moja ya mazishi eneo la Gatundu Kaskazini, kaunti ya Kiambu nchini Kenya na kuua mmoja wa waombolezaji.

Katika kisa hicho kisichokuwa cha kawaida, kilichotokea siku ya Jumamosi, Septemba 25, 2021 marehemu Mungai Mburu ambaye ni mzee wa kijiji, alikuwa amehudhuria hafla ya mazishi ya mjukuu wake wakati nyuki hao wenye hamaki walimvamia.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, mke wake marehemu, Wanjiku Mburu, baada ya maombi kufanywa kwenye kaburi, nyuki waliwavamia huku kila mmoja akichana mbuga kuokoa maisha yake.

Wanjiku alielezea kuwa ni katika taharuki hiyo ndipo mume wake aliyekuwa na umri wa miaka 85, alianguka chini baada ya kusukumwa na umati wa watu na kukumbana na mauti yake mikononi mwa nyuki hao.

Juhudi za wasamaria wema kujaribu kuokoa maisha yake hakizikufua dafu kwani alithibitika kufariki alipofikishwa katika Hospitali ya Igegania.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com