Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merisone Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kwamba Heriko alimnunulia pombe mpenzi wake Felista kwa makubaliano ya kuondoka naye lakini baadaye mwanamke huyo aliondoka na mwanaume mwingine ambaye naye alielezwa kumnunulia pombe pia, jambo ambalo lilimtia hasira Heriko na kuamua kwenda kuichoma nyumba ya mpenzi wake huyo.
Katika tukio jingine, mtu mmoja anayefahamika kwa majina ya Isaka Yustin mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa kijiji cha Emango kilichopo Kata ya Galapo wilaya ya Babati Mkoani Manyara ameuawa na aliyekuwa mkewe kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali shingoni.
Jeshi la Polisi mkoani Manyara bado linaendelea na uchunguzi kufuatia matukio hayo ya kinyama.
Social Plugin