RAIS SAMIA ATANGAZA RASMI MADIWANI KUANZA KULIPWA POSHO KILA MWEZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa serikali imeridhia madiwani kulipwa posho ya kila mwezi ili iwasaidie kuacha kuhangaika kukusanya fedha kwenye Halmashauri.

Ameyasema hayo leo Septemba 27 , 2021 akiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania-ALAT, unaofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center, Jijini Dodoma.

“Kwenye bajeti ya mwaka huu, Serikali imeridhia madiwani kuanza kulipwa posho ya kila mwezi, na hii itasaidia madiwani kuacha kuhangaika na pesa inayokusanywa kule ili wajilipe posho, posho yenu sasa imehakikishwa ipo”,amesema Rais Samia.

“Kwa kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa ukiongezeka tutaangalia kuboresha maslahi ya madiwani na watendaji wengine kwenye halmashauri zetu”, ameongeza Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post