Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa anawashangaa wale wanaosema kwamba yeye hawezi kugombea urais na kusisitiza kwamba mwaka 2025 Rais mwanamke ataingia madarakani.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 15, 2021, Jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani.
"Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia.
Wanawake bado hatujaweka Rais mwanamke, rais huyu amekaa kwa sababu ya kudra ya Mungu na matakwa ya katiba, tulichochangia sisi na dada zetu na mama zetu ni ile kusukuma hadi mwanamke akawa makamu wa Rais ule ndio mchango mkubwa tulioufanya wanawake, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana",amesema Rais Samia
“Sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana tukimweka rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana",ameongeza
Samia aliapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli. Kabla ya kupokea kijiti hicho, Samia alikuwa makamu wa Rais wa Tanzania.
Social Plugin