Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIRI 5 AMBAZO MWANAMKE HAPASWI KUMWAMBIA MUME WAKE HATA KAMA ANAMPENDA KIASI GANI


Ndoa ni muhimu, na huwa muhimu kwasababu ni kitu kinachowaunganisha mume na mke na kuanzisha familia, na huleta baraka nyingi kama vile watoto na nyinginezo nyingi.

Hatahivyo siku hizi, ndoa nyingi huishia kuvunjika kutokana na sababu moja au nyingine, hususan kutokana na ugomvi ndani baina ya wanandoa.

Bila shaka haipaswi kuwa siri baina ya wanandoa, lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo mwanamke hapaswi kumwambia mume wake, hata kama wanapendana kiasi gani.

Katika jamii nyingi za kiafrika kuna msemo usemao, maskio yasiposikia , moyo hauwezi kukasirika. Na kama tunataka amani ndani ya familia lazima kutakuwa na matukio magumu , na mwanamke anapaswa kusaidia katika utatuzi wa mambo hayo.

Yafuatayo ni mambo 5 ambayo mwanamke hapaswi kumwambia mume wake:

1. Idadi ya wanaume uliojamiana nao kabla ya kuoana na mume wako

Hupaswi kumfahamisja mpenzi wako wa kiume au mume wako ni wanaume wangapi ulikutana nao kimwi kabla ya kuishi naye.

Swababu ni kwamba unaweza kufikiri hautamkose mume wako siku sijazo. Na kama idadi ya wanaume uliyomwambia ni wengi anaweza kufikiri wewe ni kahaba au mzinzi.

Kwahiyo, iwapo atakuuliza ni wanaume wangapi ulishawahi kukutana nao kimwili, unaweza kucheka tu na umwambie :''Ebu wacha tunachane na hayo, lakini swala la ni wangapi halihusiani na safari ya mapenzi. Hebu njoo ".

2. Kusema siri za mpenzi wako wa kiume au mume wako wakati mmoja


Ukiulizwa maswali kumuhusu mwanaume, mujibu machache

Usiseme mambo ambayo yanaweza kumfanya mume au mpenzi wako ahisi kwamba sio bora vya kutosha, au ajihisi kuwa mtu mbaya

Usizungumzie kuhusu -ungependa kuwa na uhusiano na mwanaume tajiri kiasi fulani, mwenye uwezo wa kingono kiasi gani, na ni kwa vipi ungependa ampende mke wake, kwa mume mpya.


3. Usimwambie mume wako kwamba unampenda sana rafiki yako au shemeji yako

Sote tunafahamu kuwa inawezekana kwa rafiki au shemeji kutaka kukuoa.

Lakini, ni hatari kumwambia mume wako kuhusu wazo hili . Sababu ni kwamba mume wako anaweza kuanza kuwa na mashaka kuhusu tabia zake na vitendo vyako kumuhusu mwanaume huyo, jambo linaloweza kusambaratisha ndoa yako.

4. Usijaribu kumwambia kuwa unamchukia mama yake au familia yake

Hata mama mkwe awei mtu nmbaya kiasi gani, usimwambie mume wako kuwa unamchukia. Au unaichukia familia yake. Hata kama umekasirika kiasi gani, usijaribu kusema mambo mabaya kuwahusu, au kumuona mume wako sawa na familia yake.

Kama hauepatani na yeyote katika familia ya mume wako, elezea kwa utulivu, ukiwa na matumaini kuwa ataelewa ni kwanini haupatani nao.

Mume wako pia ataweza kukusaidia kutatua tatizo, na pia itazuwia matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi.

5. Usimtishe mume wako kuwa utakuja kutalikiana naye

Siku utakapomwambia mume wako kuwa utaachana naye wakati mnazozana, jua ndio mwanzo wa malumbano ndani ya ndoa.

Ndoa itaanza kukumbwa na misukosuko, wasi wasi na kutoamianiana.

Kutishia talaka katika ndoa inamaanisha kuwa hauna moyo wa imani katika ndoa, na haupatii umuhimu. Isipokuwa kama katika ndoa kuna unyanyasaji au uhalifu mwingine mbaya, ni vyema kujaribu kushirikiana kutatua changamoto zozote mlizonazo.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com