Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC KISHAPU ALIPONGEZA SHIRIKA LA TCRS KWA KUFADHILI WA MATUNDU KUMI YA VYOO SHULE YA NGOFILA


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude amelipongeza shirika la TCRS wilaya ya Kishapu kwa ufadhili walioufanya katika shule ya sekondari ya Ngofila kwa kuchangia shilingi milioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 10 ya vyoo.

Mkude ametoa pongezi hizo Septemba 3,2021 akizungumza na wananchi katika ziara ya kikazi kata ya Ngofila alipokuwa akikagua mradi huo.

"Tunawashukuru sana wenzetu wa TCRS kwa kutenga bajeti ya shilingi milioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika shule hii huu ni ungwana tunahaitajia mashirika kama haya ambayo yana mtazamo chanya kwa jamii na ambayo yapo tayari kutoa ufadhili kwenye jamii. Mimi natoa pongezi sana kwa kiasi waliochotoa kawni kinatosha kabisa kukamilisha ujenzi wa matundu hayo",amesema Mkude.

Diwani wa kata ya Ngofila Nestory Ngude  alikiri kupokea bajeti ya milioni 18 ambayo imetengwa na shirika la TCRS kwa ajili ya ujenzi wa matundu 10 ya vyoo vya kisasa.

"Nakiri tulipokea bajeti ya milioni 18 kutoka kwa kiongozi wa mradi TCRS Kishapu Oscar Lutenge katika kikao cha OCD. Katika ujenzi tunagawana majukumu kuna nguvu kazi pia ya wananchi ambayo inatumika katika ujenzi wa matundu hayo kama vile kuchimba msingi na usogezaji mchanga"

"Hata hivyo hatupokei pesa Cash ila tunaletewa vifaa vya ujenzi kwa kila hatua tunayofika",amesema

Kiongozi wa mradi TCRS Kishapu Oscar Lutenge amesema walipokea barua ya maombi ya kufadhili ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kupitia vikao vya OCD na kukubali kufadhili mradi huo kwa bajeti ya shilingi milioni 18 ambayo imetolewa  na shirika la TCRS ambalo limehudumu katika kijiji cha Ngofila zaidi ya miaka 10

“Tulipokea barua ya maombi kupitia kiakao cha OCD kwajili ya kufadhili ujenzi wa matundu 10 ya vyoo vya kisasa katika sekondari ya Ngofila ,hii ni kwa sababu ya sisi kufanya kazi na kijiji cha Ngofila zaidi ya miaka 10, na katika bajeti yetu hatutoi pesa bali tunaleta vifaa vya ujenzi kwa kila hatua , hatuwezi kuleta mifuko 100 kwa mkupuo , kwa sababu tunaepusha matumizi mabovu ya vifaa hivyo”, aliongeza.

"Japo tumechelewa kuanza ujenzi na tupo nyuma ya mwaka wa fedha lakini tunapambana tumalize ujenzi mapema iwezekanavyo kulingana na ushirikianao wa wananchi”,alisema

"Tuna sehemu nyingi ambazo tumetoa ufadhili katika wilaya ya Kishapu japo hatuna uwezo wa kufadhili Kishapu nzima lakini angalau kila awamu tunajitahidi angalau tunagusa sehemu mbalimbali",alieleza 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com