Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA : TOZO ZA MIAMALA YA SIMU ZITAENDELEA KUWEPO KAMA KAWAIDA


Rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa tozo za miamala ya simu zitaendelea kuwepo kama kawaida ili kupata fedha za kuendeleza miradi ya maendeleo na kujiepusha kuwa kwenye mikono ya wafadhili.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 2, 2021, wakati akiwasalimia wananchi wa Tegeta akiwa njiani kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya kurekodi vipande vya filamu vitakavyotangaza utalii wa Tanzania kimataifa, filamu ambayo itazinduliwa nchini Marekani.

"Nataka niwaambie kwamba tozo zitaendelea kuwepo na sitaki kuwaficha, kwa sababu tozo zile miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya zaidi ya shilingi bilioni 60 na zimepelekwa kujenga vituo vya afya 220 hivyo tunajenga wenyewe ili wafadhili wanaokuja na masharti wasituingilie mambo yetu," amesema Rais Samia.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com