Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya akizungumza wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) leo Jumatatu Septemba 20,2021 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya akionesha Mpango Mkakati wa Mkoa katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Mratibu wa Masuala ya Jinsia Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwajina Lipinga ambaye pia ni Mratibu wa MTAKUWWA Ofisi ya Rais TAMISEMI akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA)
Mratibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA)
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakiwa ukumbini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya aliyekuwa ameambatana na Mratibu wa Masuala ya Jinsia Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwajina Lipinga ambaye pia ni Mratibu wa MTAKUWWA Ofisi ya Rais TAMISEMI amefanya kikao hicho leo Jumatatu Septemba 20,2021 Mjini Shinyanga kikiwa na lengo na kufuatilia utekelezaji wa MTAKUWWA mkoani Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hicho, Mmuya amewataka wadau yakiwemo mashirika na taasisi zisizo za Kiserikali kushirikiana na Serikali katika kuondoa mila na desturi Kandamizi ambazo amesema ndiyo zimekuwa zikichangia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii.
“Mila na desturi kandamizi katika maeneo mengi ndiyo inachangia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Mila hizi tunaziendekeza sisi kwa kufanya vikao ngazi ya familia na kumaliza kesi za ukatili kienyeji. Tunalipana fedha na mali na kumaliza kesi za matukio badala ya kupeleka kesi kwenye vyombo vya sheria huku vyombo vya sheria navyo vikilaumiwa kuchelewesha maamuzi matokeo yake ushahidi unapotea na matukio yanaendelea kutokea kwani hakuna hatua kali zinazochukuliwa kwa wahusika”,amesema Mmuya.
Mmuya ametumia fursa hiyo kuiomba jamii kuacha kumaliza kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kifamilia na kuvishauri vyombo vya dola ikiwemo Polisi na Mahakama kukaa na kujadili namna ya kuondoa changamoto ya ucheleweshaji wa kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Rai yangu kwa wadau,nyinyi mmebeba rasilimali fedha, rasilimali watu na ujuzi na mnaisaidia sana serikali. Kinachotufurahisha zaidi nyinyi mnakutana na wananchi moja kwa moja. Naomba mshirikiane, mtambuane, mjadili kwa pamoja masuala yanayohusu wananchi kisha mgawane maeneo ya kazi badala ya wadau wengi kujikita katika eneo moja”, amesema Mmuya.
“Tunataka Rasilimali chache zitumike kwa matokeo makubwa katika kuhakikisha tunatokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo kuondoa sifa mbaya ya kuwa na mimba na ndoa za utotoni”,ameongeza Mmuya.
Aidha amewataka Maafisa Maendeleo ya jamii kutimiza majukumu yao kikamilifu kwani serikali inataka kaya/familia zitoke kwenye hali ya kuomba omba zianze kuzalisha mali, uchumi ngazi ya kaya upande ili kuongeza tija ya uchumi wa nchi.
Katika hatua nyingine ameuongeza Mkoa wa Shinyanga kwa kutengeneza Mpango Mkakati wa Mkoa katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ifikapo mwaka 2025 ambao umekuwa chachu ya mabadiliko katika mkoa wa Shinyanga.
“Shinyanga mnaendelea kufanya vizuri katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia lakini bado mna fursa ya kufanya vizuri zaidi. Niwapongeze wadau mmekuwa na ushirikiano mzuri na serikali”,amesema.
Mratibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale amesema Serikali ya mkoa ni ya kwanza hapa nchini kati ya mikoa 26 , kuzindua mpango wake mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano, kuanzia (2020-2025) kwa kuonyesha dira ya mkoa na kubainisha changamoto zilizopo katika mkoa ambazo ni chanzo cha matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuzifanyia kazi.
Mratibu wa Masuala ya Jinsia Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwajina Lipinga ambaye pia ni Mratibu wa MTAKUWWA Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema ni jukumu la kila mratibu wa MTAKUWWA kila eneo lake kutambua wadau wa kushirikiana nao badala ya majukumu kuachiwa majukumu yote na kutekeleza MTAKUWWA.
Nao Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapa ushirikiano katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii yakiwemo matukio ya ukatili wa kijinsia.
Akiwa katika kikao hicho ,Naibu Katibu Mkuu huyo Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya amekabidhi vyeti kwa baadhi ya wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele katika masuala ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
Mmuya amewataja wadau hao kuwa ni Shirika la ICS, WFT, Save The Children, Thubutu Africa Initiative, Agape Aids Control Programme, FHI 360, Msichana Initiative, UNFPA,REDESO,PACESH, TCRS,SHIDEPHA + na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC).
Wengine ni Dr. Machiya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mary Urio,Hakimu Mfawidhi wilaya ya Shinyanga Mhe. Ushindi Swalo,Mwendesha Mashtaka Mkoa, Polisi Dawati la Jinsia na Watoto na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Ushetu Bw. Morgan Kichere.
Social Plugin