Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA FREEDOM HOUSE YAAHIDI KUFANYA KAZI NA SERIKALI KWENYE HAMASA YA CHANJO YA UVIKO 19

Na Richard Edwin -Mwanza
Mkurugenzi wa Taasisi ya Frredom House Bwana Daniel Lema amesema taasisi hiyo inaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuhimiza wananchi kupata chanjo ya UVIKO 19 na taasisi hiyo ipo tayari kufanya kazi pamoja na Serikali.

Bwana Lema amesema hayo wakati akifunga majadiliano ya kimtandao yaliyowakutanisha vyombo vya habari na AZAKI pamoja na wataalamu wa afya.

Bwana Lema aliweka bayana nia yake ya kufanikisha majukwaa ya majadiliano yanayowaleta wadau pamoja na kujadili juu ya umuhimu wa watanzania kupata chanjo ya UVIKO 19 ili kulinda afya zao.

Freedom House kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza waliandaa mkutano wa mtandaoni na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mwenendo wa chanjo ya UVIKO 19.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza Bwana Edwin Soko alisema mijadala ni muhimu kwenye kuondoa dhana potofu juu ya chanjo ya UVIKO 19.

Soko aliongeza kuwa, majadiliano hayo yalilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari pamoja na AZAKI ili waweze kutimiza vyema majukumu yao kwa kuhakikisha wananchi wanapewa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa chanjo.

Mgeni rasmi kwenye majadiliano hayo ya kimtandao alikuwa ni Mkurugenzi wa kitengo cha Kinga Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi.

Dkt. Subi aliIishukuru Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza na Freedom House kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali na kupata elimu ya umuhimu wa chanjo.

Majadiliano hayo yalifanyika Septemba 10 mwaka huu kwa njia ya mtandao na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki mia moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com