Na Frankius Cleophace Serengeti.
Kituo cha watoto wenye Ulemavu cha St: Justin kilichopo Manispaa ya MusomaMkoani Mara kwa kushirikiana na Shirika la Right to Play kupitia mradi wa elimu Jumuishi kimewapatia elimu wanafunzi shule ya msingi Regicha na wazazi kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike,usawa wa kijinsia na ulinzi kwa mtoto.
Emmanuel Omenda ambaye ni Meneja Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka kituo cha watoto wenye ulemavu cha St:Justin kilichopo Musoma alisema kuwa wanatumia michezo mbalimbali kufikisha elimu hiyo nakueleza kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Regicha 498 na wazazi 60 wamefikiwa na elimu hiyo.
"Tunatumia Ngonjera, Maigizo, Mpira wa Miguu hata kwa watoto wa kike lengo nikufikisha ujumbe uliokusudiwa kupitia Mradi wa Elimu Jumuishi na Elimu hii ni endelevu tutaemdela kutoa Elimu katika kata nyingine wilaya ya Serengeti Mkoani Mara ili jamii iwezekuondokana na suala la Ukatili",alisema Emmanuel.
Kwa upande wake Afisa elimu kata ya Regicha Jumamosi Regata alisema kuwa akipongeza kituo hicho kuendelea kutoa elimu kwa wazazi na walezi pamoja na wanafunzo ili jamii iondokane na ukatili.
Aidha wanafunzi kutoka shule ya msingi Regicha iliyopo wilayani Serengeti Mkoani Mara walilisisitiza elimu hiyo kuendelea kutolewa jamii iweze kuthamini na kutambua haki za motto wa kike.
Social Plugin