Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE YANGA SC HASHIM MUHIKA AFARIKI DUNIA


Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la klabu ya Yanga, Hashim Muhika (pichani kushoto), amefariki dunia alfajiri ya leo Jumapili nyumbani kwake Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam.

Marehemu Muhika alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa kipindi kirefu, msiba wake upo Mtoni Mtongani.

Anatarajiwa kuzikwa kati ya makaburi ya maeneo matatu ya Kisiju, Mtoni Mtongani na Kisutu inaelezwa kikao kitakachokaliwa leo mchana majira ya saa 8, kitaamua.

Marehemu alifariki akiwa na umri wa miaka 87, ameacha mtoto mmoja na mjukuu mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com